Kikosi cha timu ya KMC FC kimeendelea kujifua kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu soka Tanzania bara dhidi ya Yanga ukataopigwa siku ya Jumamosi ya Aprili 10 katika uwanja wa Mkapa kuanzia majira saa moja kamili jioni (19:00).

Katika mchezo huo KMC FC inakutana na Yanga kwa mara ya pili  huku ikiwa ugenini  kwenye msimu huu wa Ligi Kuu 2020/2021.

Afisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema wamejipanga kuhakikisha kwamba kikosi chao kinaleta furaha kwa mashabiki kwa kuondoka na alama tatu hivyo wajitokeze uwanjani kutoa sapoti kwa wachezaji.

Amesema, Kino Boys inakwenda kupambania alama tatu muhimu kwenye mchezo huo ambapo katika mchezo wa duru ya kwanza walipoteza kwa goli 2-1 mechi iliyochezwa CCM Kirumba Mwanza 
KMC FC  inatafuta ushindi huo ili kujiimarisha katika msimamo wa ligi Kuu na kwamba licha ya kuwa na upinzani mkubwa wakupambania alama tatu lakini hakuna kitakachoshindikana.

“Tunakwenda kwenye mchezo ambao kimsingi hautakuwa mwepesi kutokana na aina ya timu ambayo tunakutana nayo, ni nzuri, wanafanya vizuri, lakini pia wanaongoza ligi, hivyo mchezo utakuwa mgumu lakini pamoja na yote bado KMC FC tunasema kwamba tunakwenda kupambanania alama tatu na tunaimani kubwa yakufanya vizuri kwenye mchezo wetu," amesema.

Katika msimuu huu KMC FC ilikutana na yanga Oktoba mwaka jana katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza na kupoteza mchezo huo ambapo walifunga magoli mawili kwa moja, Goli la KMC lilifungwa na Hassan Kabunda kipindi cha kwanza katika dakika ya 23.Kocha Mkuu wa Timu ya KMC FC , John Simkoko akitoa maelekezo kwa wachezaji wa Timu hiyo katika mazoezi ambayo KinoBoys wanaendelea nayo hivi sasa.Goli Kipa wa Timu ya KMC FC Sudi Dondola akiwa kwenye mazoezi ya kujifua kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga hapo Jumamosi.
wachezaji wa Timu ya KMC FC wakiwa kwenye mazoezi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...