Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

MWANASIASA Maarufu nchini Mexico  Carlos Mayorga ameingia katika mijadala mbalimbali baada ya kuzindua kampeni zake za Ubunge akiwa ndani ya jeneza France24 imeripoti.

Carlos Mayorga alitumia njia hiyo kuonesha hali halisi ya taifa hilo ambalo mamia ya watu wanakufa kutokana na virusi vya Corona pamoja na vurugu zinazohusiana na biashara.

Akiwa mgombea kutoka chama cha Encuentro Salidario kusini mwa jimbo la Chihuahua Mayorga alisema, alifikia uamuzi huo kwa malengo ya kufikisha ujumbe kwa wanasiasa ambao wanasababisha watu kupoteza maisha kutokana na kutojali kwao.

Mwanasiasa huyo aliwasili katika kampeni zake katika daraja linalotengenesha mji wa wa Ciudad Juarezy na El Paso Texas akiwa ndani ya jeneza la rangi ya fedha.

 Carlos Mayorga aliambatana na wasaidizi waliovaa mavazi na vifaa vya kujilinda wakiwa na mashada ya maua kama ishara ya kupaza sauti juu ya janga hilo ambapo hadi sasa watu 200,000 wamefariki nchini humo kutokana na Covid-19.

Vyombo vya habari vilimnukuu mwanasiasa huyo akisema;

"Wanasiasa wameendelea kukaa kimya wakati matukio ya uhalifu yakiendelea, na wameendelea kukaa kimya kuhusu hali mbaya ya Covid-19." Alinukuliwa.

Zaidi ya watu 300,000 wameuawa nchini Mexico tangu Serikali itoe nguvu kwa jeshi katika kupambana na vita dhidi ya dawa za kulevya 2006 kwa mujibu kwa taarifa rasmi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...