Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiweka Shada la Maua katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume mara baada ya Dua iliyofanyika katika Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui Zanzibar leo tarehe 07 April 2021 katika Siku ya Kumbukumbu ya (Karume Day).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, pamoja na Viongozi wengine wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiomba Dua mbele ya Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume katika Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar leo tarehe 07 April 2021 katika Siku ya Karume Day.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa mara baada ya Dua Maalumu ya kumuombea Rais wa Kwanza
wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume katika siku ya Kumbukumbu ya
Karume (Karume Day) iliyofanyika leo tarehe 07 April 2021 katika Ofisi
Kuu za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar.
Mhe Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui mahali alipozikwa Hayati Rais Abeid Amani Karume Rais wa kwanza wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar , ambapo leo imefanyika Dua maalum ya kumuombea katika siku ya kumbukumbu yake.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi Mhe Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwasili ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui mahali alipozikwa Hayati Rais Abeid Amani Karume,Rais wa kwanza wa serikali ya mapinduzi Zanzibar ambapo leo imefanyika Dua maalum ya kumuombea katika siku ya kumbukumbu yake.
Mhe rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Dua maalumu ya kumuombea Hayati rais Abeid Amani Karume Rais wa kwanza wa serikali ya mapinduzi Zanzibar katika siku ya kumbukumbu yake. katika ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui mahali alipozikwa,leo April 7, 2021 .
Mhe Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mjane wa Hayati Rais Abeid Aman Karume Mama Fatuma Karume , wakati alipowasili kwenye Dua maalumu ya kumuombea Hayati Rais Abeid Amani Karume,Rais wa kwanza wa serikali ya mapinduzi Zanzibar katika siku ya kumbukumbu yake. katika ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui mahali alipozikwa,leo April 7, 2021 .
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ,Mke wa Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanziba Dkt. Hussein Ali Mwinyi , Mama Mariam Mwinyi, na Katibu mkuu Kiongozi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said wakishiriki Dua maalumu ya kumuombea Hayati Rais Abeid Amani Karume,Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika siku ya kumbukumbu yake, katika ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui mahali alipozikwa, leo April 7, 2021 .
PICHA NA IKULU
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...