Na Mwandishi Wetu- Mbeya
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeteketeza bidhaa hafifu za vyakula na vipodozi zenye thamani ya shilingi milioni 19 katika maeneo mbalimbali ya biashara katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Kwa Mujibu wa Meneja wa Shirika hilo Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw. Abel Mwakasonda, bidhaa hizo hafifu zilikamatwa wakati wa ukaguzi wa bidhaa sokoni uliofanyika katika kipindi cha Januari hadi Machi, 2021 katika mikoa ya Iringa, Njombe, Songwe na Mbeya.

“Bidhaa hizo ni pamoja na vinywaji aina ya soda,bia, vyakula kama biskuti,mafuta ya kula, siagi na sabuni za kuogea ambazo muda wake wa matumizi umekwisha”, inaeleza taarifa hiyo.

Vilevile vipodozi vilivyokamatwa ni vile visivyoruhusiwa kuingizwa hapa nchini kutokana na kuwa na viambata sumu kama vile madini tembo (lead), zebaki (Mercury) na Hydroquinone.

Matumizi ya vipodozi hivyo vyenye viambata sumu yana madhara kiafya ambayo husababisha magonjwa ya saratani kwa binadamu, na kwamba, vyakula vilivyokwisha muda wa matumizi husababisha magonjwa ya homa za matumbo.

Aidha, Taarifa hiyo inaeleza kuwa matumizi ya bidhaa hafifu huleta madhara ya kiuchumi kwa muuzaji na mnunuzi wa bidhaa husika baada ya kuthibitishwa kuwa bidhaa hizo hazifai kwa matumizi ya binadamu na kutakiwa kuondolewa sokoni na kuharibiwa.

Ukaguzi wa bidhaa sokoni unafanywa kwa kuzingatia sheria ya Viwango Na 2 ya mwaka 2009 na Sheria ya Fedha Na 8 ya mwaka 2019 ambayo ilihamisha majukumu ya usajili wa majengo ya vyakula na vipodozi yaliyokuwa yakifanywa na iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwenda kwa TBS.

Shirika linatoa rai kwa wauzaji wa bidhaa mbalimbali kuhakikisha kuwa wanaingiza sokoni bidhaa ambazo TBS imethibitisha ubora wake na kuziondoa sokoni bidhaa zilizokwisha muda wake wa matumizi badala ya kuendelea kuziuza.Tingatinga likitetekeleza bidhaa hafifu zilizokamatwa katika mikoa ya Nyanda za Juu kusini kufuatia ukaguzi uliofanywa na Shirika la Viwango Tanzani (TBS ) katika mikoa hiyo kati ya Januari na Machi, 2021.Bidhaa hafifu zikishushwa katika eneo la utekekezaji katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini baada ya kukamatwa kufuatia ukaguzi uliofanywa na Shirika la Viwango Tanzani (TBS ) katika mikoa hiyo kati ya Januari na Machi, 2021.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...