Watuhumiwa wakiwa wakitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo mara baada ya kusomewa mashtaka mbele ya Mahakimu wawili tofauti kujibu mashtaka nane yakiwemo ya kuingiza na kusimika vifaa vya mawasiliano bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Watuhumiwa wakiwa wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Mahakimu wawili tofauti kujibu mashtaka nane yakiwemo ya kuingiza na kusimika vifaa vya mawasiliano bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Watuhumiwa wakiwa wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Mahakimu wawili tofauti kujibu mashtaka nane yakiwemo ya kuingiza na kusimika vifaa vya mawasiliano bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

WATU wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Mahakimu wawili tofauti kujibu mashtaka nane yakiwemo ya kuingiza na kusimika vifaa vya mawasiliano bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) pamoja na kuisababisha Serikali ya Tanzania hasara ya Sh. milioni.69

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Ester Martin akisaidiana na Adolf Ulaya na Adolf Lema imewataja washtakiwa hao kuwa ni Hemed Hemed(22), Daud Kalombe(31) na Lucas Nkunguru(29) na Jeremiah Laizer .

Washtakiwa walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kuongoza genge la uhalifu kwa kuratibu shughuli za kihalifu; kuingiza vifaa vya mawasiliano bila kuwa na kubali cha TCRA; kusimika vifaa vya mawasiliano Tanzania na kuendesha mitambo ya Mawasiliano bila kuwa na kibali.

Pia kutumia vifaa vya mawasiliano bila kudhibitisha na TCRA; matumizi ya kilaghai ya vifaa vya mawasiliano; kuisababisha hasara Serikali na TCRA pamoja na kutakatisha fedha kiasi cha Sh 69, 690,000.

Mbele ya Hakimu Chaungu imedaiwa kati ya Desemba Mosi, 2020 na Februari 22, 2021 katika maeneo Dodoma, Mbeya na Dar es salaam, washtakiwa walipanga kujipatia faida kwa kuratibu shughuli za kihalifu.

Imeendelea kudaiwa kuwa, katika siku na Mikoa hiyo, kwa matendo yao ya kihalifu washtakiwa waliisababishia Serikali na TCRA hasara ya Sh. milioni 69

Aidha, katika shtaka la kutakatisha fedha, inadaiwa katika kipindi hicho na maeneo hayo hayo washitakiwa huku wakijua kuwa fedha hizo ni zao tangulizi la uhalifu na matumizi ya kilaghai ya kukwepa tozo ambazo zingelipwa kwa ajili ya kusambaza mawasiliano, walijipatia Sh. Milioni 69

Mbele ya Hakimu Mmbando inadaiwa, kati ya Januari Mosi 2021 na Machi 6, 2021 katika mikoa ya Dodoma na Songwe, washtakiwa Jeremiah Laizer na Daud Kambole wanadaiwa kupanga njama ya kujipatia faida kwa kuratibu shughuli za kihalifu.

Shtaka la pili, Februari 2, 2021 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, waliingiza vifaa vya mawasiliano bila kuwa na leseni ya TCRA.

katika shtaka la kutakatisha fedha, Laizer anadaiwa kutenda kosa hilo Februari 28, 2021 na Machi 5, 2021 katika eneo la Tunduma mkoani Songwe, anadaiwa kujipatia fedha kiasi Sh 19, 734, 000 .

Pia wanadiawa kuisababisha Serikali hasara ya sh. Milioni 19.

Kesi zote zimeahirishwa hadi April 27, 2021 Washtakiwa wamerudishwa rumande.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...