Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel Money leo imezindua kampeni maalum itakayojulikana kama ‘’Airtel Money Tunakuunganisha na Dunia’ ambapo itawawezesha wateja wote wa Airtel Money kupokea fedha kutoka nchi Zaidi ya 200 duniani moja kwa moja kupitia akaunti zao za Airtel Money.
Akizungumza jijiji Dar es Salaam leo wakati wa kuitangaza kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda alisema “huduma ya kupokea fedha kutoka nchi zaidi ya 200 itajulikana kama Airtel Money Tunakuunganisha na Dunia” hakuna mipaka wala changamoto ya kupokea fedha kutoka nje ya nchi ukiwa na Airtel Money sasa”
“Huduma hii ni inadhihirisha dhamira yetu ya kuendelea kushirikiana na serikali ili kuleta suluhisho la huduma za kifedha hapa nchini ili kuwafikia Watanzania wengi ambao bado hawajafikiwa na huduma za kibenki. Tunaelewa ya kwamba tunao ndugu, jamaa na marafiki walio nje ya nchi ambao wangependa kutuma fedha kwa ndugu zao watanzania lakini wanakumbana na vikwazo kutokana na hatua nyingi zinazotakiwa wakati wa kutuma fedha nje ya nchi. Airtel Money imekuja na suluhisho, mteja wa Airtel Money anatakiwa kuw na laini ya simu ya Airtel ambayo imesajiliwa tu”. Nchunda alisema.
Nchunda aliongeza kuwa Airtel Money Tunakuunganisha na Dunia itaboresha uchumi shirikishi kati ya familia na marafiki waliopo nje ya nchi kwa kuwa itaongeza uhuru wa kuchangua njia rahisi na ya haraka pale inapohitaji kupokea fedha au kwa wanaotaka kutuma fedha hapa nchini kwa haraka, huku sisi Airtel tukiwa tumejipanga kikamilifu kuendelea kutoa huduma nafuu, salama, haraka bila mipaka.
Nchunda alizitaja baadhi ya nchi ambazo mteja wa Airtel Money ataweza kupokea fedha moja kwa moja kwenye akaunti yake ya Airtel Money ni pamoja na Marekani, Uingereza, Ujerumani, Uswizi, Swedeni, Uholanzi, Italia, Norway pamoja na nchi zote za Afrika Mashariki.
“Mnamo mwishoni mwa mwaka jana, Airtel kwa kushirikiana na WorldRemit, ambayo ni kampuni ya kimataifa ya malipo walizindua mfumo huu wa malipo kwa kuwawezesha wateja wa Airtel Money kupokea fedha moja kwa moja kwenye akaunti zao za Airtel Money kwa nchi Zaidi ya 50. Huu ni muendelezo wa kuhakikisha wateja wetu wanaishi kwenye dunia ya kisasa pamoja na kwenda na mabadiliko ya teknolojia kwenye upande wa kutuma na kupokea fedha kimtandao’, alisema.
“Lengo letu kama kampuni siku zote imekuwa ni kutoa huduma na bidhaa ambazo ni za kipekee na ambazo zinapatikana kwa unafuu ili kuendana na maisha ya kila siku ya wateja wetu. Kwa kuzindua pokea fedha kutoka nchi Zaidi ya 200, tunaileta pamoja jamii kwa kuondoa mipaka kwani wote wataweza kupokea fedha moja kwa moja kwenye akaunti zao za Airtel Money kutoka mataifa mbalimbali’, Nchunda aliongeza.
Airtel Money ni moja ya huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi ambayo inakuwa kwa kasi huku ikiwa hapa nchini ikiwa imeunganisha na makampuni ya malipo ya huduma mbalimbali zaidi ya 1000, pamoja na kuunganisha na taasisi za fedha zaidi ya 40. Vile vile, Airtel Tanzania inazidi kupanua wigo kupitia Airtel Money Branch karibu yako ambapo kwa sasa ina maduka ya Airtel Money Branch zaidi ya 1200 ambayo yanatoa huduma na bidhaa zote za Airtel nchni.

Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando kulia akiwa na Mkurugenzi wa Airtel Money Isack pamoja na Mkuu wa Chapa wa Airtel Money bi Gilian Rugumamu wakizindua rasmi kampeni maalum itakayojulikana kama ‘’Airtel Money Tunakuunganisha na Dunia’ ambapo itawawezesha wateja wote wa Airtel Money kupokea fedha kutoka nchi Zaidi ya 200 duniani moja kwa moja kupitia akaunti zao za Airtel Money.

Meneja Uhusiano Airtel Jackson Mmbando (kulia) akiongea na waandishi wa habari leo wakati kuzindua kampeni maalum itakayojulikana kama ‘’Airtel Money Tunakuunganisha na Dunia’ ambapo itawawezesha wateja wote wa Airtel Money kupokea fedha kutoka nchi Zaidi ya 200 duniani moja kwa moja kupitia akaunti zao za Airtel Money. Kushoto ni Mkurugenzi wa huduma za Airtel Money.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...