Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.

TAMASHA kubwa la kibiashara la Holiday Market Festival linatarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza 20 hadi 23 Mei mwaka huu katika viunga vya hoteli ya Verde, Unguja, Zanzibar.

Akielezea maandalizi ya tamasha kwa vyombo vya Habari, Meneja matukio wa Holiday Market, Bi. Raiyan Mohamed Rashid  amesema Wafanyabiashara zaidi ya 100 wanatarajiwa kushiriki kuuza bidhaa mbalimbali za ndani na nje sambamba na uwepo wa kongamano la uchumi wa bluu.

"Tamasha hili kwa mara ya kwanza tunatarajia kuunganisha  wafanyabishara toka sehemu tofauti wa hapa Visiwa vya Zanzibar, Tanzania Bara na wale wa ndani na nje ya Tanzania.

Tukiwa na lengo la kuleta hamasa kwenye kipindi cha kuelekea kwenye mapumziko ya mwenzi wa sita (Juni)." Alisema Meneja matukio Bi. Raiyan Mohamed Rashid.

Aliongeza kuwa: Taasisi za Serikali na zisizo za Kiserikali, kampuni, Hoteli, kampuni za Utalii  na zingine pamoja na watu binafsi zitakusanyika kwa pamoja kuonyesha na kuuza kwa bei nafuu zaidi katika kusheherekea kwa pamoja.

"Tunazikusanya pamoja ili kuonyesha na kuuza kwa bei nafuu zaidi na tutasherehekea kwa pamoja hiyo tarehe 20 mpaka 23 Mei 2021 katika Hoteli ya Verde iliyopo hapa Unguja, Zanzibar." Alieleza Meneja matukio Bi. Raiyan Mohamed Rashid.

Aidha aliongeza kuwa, wameungana  na ZATO ( Zanzibar Association of tour Operators ) ili kuleta utofauti kwenye tamasha hilo ambapo pia ametoa wito kwa wafanyabiashara kujitokeza kuchangamkia fursa za kukodi mabanda.

"Tukiwa hatua ya mwisho ya tamasha letu pia bado tunawakaribisha sana ambao wanahitaji kushirikiana nasi kwenye kukodi mabanda bado yapo kwa bei nafuu." Meneja matukio, Bi. Raiyan Mohamed Rashid.

Tamasha hilo pia litaendesha jukwaa ambalo litazungumzia Utalii pamoja na uchumi wa Zanzibar kwa kuangazia uchumi wa bluu kwenye sera ya Rais Dr. Hussein Ali Mwinyi.

"Rais Dr. Hussein Mwinyi katika sera yake ni kutaka Zanzibar hiwe kwenye maendeleo ya Uchumi wa bluu nasi tutaendesha jukwaa hilo maalum kwa siku mbili.

Wanafunzi wa Vyuo na Wafanyakazi wanakaribishwa kujiunga kwenye jukwaa la Utalii na Uchumi wa bluu wakati wa tamasha" Alimalizia Meneja matukio, Bi. Raiyan Mohamed Rashid.

Meneja matukio wa Holiday Market, Bi. Raiyan Mohamed Rashid.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...