kampuni ya mawasiliano ya China ya Huawei imetoa wito wa uwepo wa ushirikiano madhubuti baina ya sekta za umma na sekta binafsi ili kurejesha imani baina ya sekta hizo mbili kwa mustakabali mzima wa uboreshaji wa teknolojia.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Makamu Mwandamizi wa Rais na mwanachama wa bodi ya wakurugenzi ya Huawei, Catherine Chen kwenye  Kongamano la Mtakatifu Gallen - mkusanyiko wa viongozi wa sasa na wa baadaye kutoka kote ulimwenguni ambao hufanyika kila mwaka.

Kongamano hilo lililenga kusherehekea kumbukumbu ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake. Katika kongamano hilo, jumla ya watu 1,000 walishiriki kwenye mazungumzo ya siku tatu baina ya vizazi tofauti kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Gallen, kituo cha kimataifa Singapore, Balozi kumi za Uswizi kote ulimwenguni, na mahali pengine mtandaoni.

Wasemaji wengine kwenye kongamano hilo ni pamoja wakuu mbalimbali kutoka sekta binafsi ambao ni pamoja na Christophe Franz, Mwenyekiti wa bodi ya Roche, Ola Källenius, Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi huko Daimler, Satya Nadella, Afisa Mtendaji Mkuu wa Microsoft, na Roshni Nadar Malhotra, Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika la HCL.

Washiriki, ambao pia walijumuisha viongozi wa kisiasa, kama vile Kansela wa Austria, Sebastian Kurz, na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, kama Mwenyekiti wa mpango wa kidijitali Uswizi, Doris Leuthard, walikusanyika kubadilishana maoni yao juu ya mada ya kongamano la mwaka huu, "Uaminifu ni Muhimu" kitu ambacho Huawei imejitolea sana.

Kwa mujibu wa Bi Chen anaamini inahitajika juhudi za pamoja za watunga sera, wasimamizi, na sekta binafsi. "Kwa kua vifaa vingi vinajumuisha mawasiliano, uwepo wa ongezeko la huduma kwa njia za mitandao pamoja na miundombinu muhimu kutegemea upatikanaji wa data kwa wakati halisi, ni lazima kwa serikali zote ulimwenguni kuhakikisha kuwa kila mtu analindwa kwa kiwango cha juu kabisa kiusalama. Kitu pekee kinachoweza kuleta imani katika teknolojia ni uwepo wa sheria moja na jumuishi kwa nchi zote.” Alisema.

Kongamano hilo kwa mwaka huu lilianza Mei 5. Washiriki wa hafla hiyo walikubaliana kwamba uaminifu hujengwa kwa uwazi, na kwamba ni wakati wa kuchukua hatua madhubuti kushughulikia changamoto hiyo na hatari ambazo zimeibuka baada ya janga la COVID-19.

Uaminifu wa umma katika taasisi za kisiasa na kiuchumi, teknolojia zinazoibuka, na vyombo vya habari vimeharibiwa hivi karibuni, haswa kati ya kizazi cha vijana, na hii imezidishwa na janga la COVID-19.

"Sisi, kwa kizazi chetu, tunaunganishwa na idadi kubwa ya watu kupitia mitandao ya kijamii, lakini hii haimaanishi ni kundi la watu ambao tunaweza kuwaamini," alisema Simon Zulliger, mshiriki wa timu ya wanafunzi 35 kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Gallen ambacho kiliandaa kongamano la mwaka huu. Timu hiyo ilielezea maoni yao kuwa kutafuta njia za kuhifadhi na kuimarisha uaminifu ni muhimu kwa kurudisha imani.

Chen anatumaini kwamba kizazi kijacho cha viongozi kitaunda uaminifu na kuunda ulimwengu uliounganishwa kimtandao. "Ninawahimiza waendelee kukuza uhusiano mzuri kati ya jamii, watu, na mazingira yao. Lazima tujenge imani kubwa katika teknolojia, iliyowezeshwa na ya sheria jumuishi, ubunifu na maendeleo. Hapo tu ndipo tunaweza kujitolea kwa matumizi endelevu na ya kuaminika ya teknolojia." alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...