INSPEKTA Jenerali wa Polisi Simon Nyakoro Sirro amemuapisha ACP S.R.Hamdun kuwa Kamishna wa Polisi katika ukumbi wa Mikutano Makao makuu ndogo jijini Dsm.

kiapo hicho kimekuja baada ya  Mhe,  Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumteua ACP Hamdun kuwa Kamishna na Mkurugenzi wa Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa(PCCB).

IJP Sirro amempongeza CP Hamdun kwa weledi aliouonyesha katika utumishi wake ndani ya Jeshi la Polisi hasa alipokuwa Kamanda wa Polisi katika mikoa ya Ilala, Njombe, Kilimanjaro, Arusha na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum Dar es salaam.

Aidha CP- SALUM RASHID HAMDUN amemshukuru Mhe, Rais kwa kumuamini katika nafasi hiyo. Pia amelishukuru Jeshi la Polisi kwa nafasi alizopata na kuzifanyia kazi kwa weledi mkubwa. Amesema katika kazi mambo makubwa ni USIMAMIZI mzuri wa kazi, NIDHAMU na UADILIFU  ni nyenzo muhimu katika utendaji wetu wa kazi za kila siku.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...