Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Isaya Mwakifulefule akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Shirika hilo kudhamini Bima Marathon zitazofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Bima Marathon Baraka Mtavangu akizungumza namna walivyoipokea udhamini wa NIC katika kutanikisha marathon zitazotimua vumbi jijini Dar es Salaam.
 


*Fedha zitakazopatikana kwenda kwa watoto njiti

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC)  limekuwa mdhamini mkuu wa mbio za Bima marathon zitakazofanyika Mei 29 mwaka huu katika uwanja cha Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Marathon hizo zimelenga kukusanya fedha kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuzuia  vifo vya watoto njiti na kuimarisha afya zao kwa fedha hizo kununua vitanda maalum.

Hayo yamebainishwa Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja wa NIC Isaya Mwakifulefule wakati akizungumza na  waandishi wa habari  kuhusiana na udhamini wa marathon hizo.

 Amesema kuwa NIC wamekuwa mstari wa mbele kusapoti mambo mbalimbali yenye tija na  lengo la kukuza ajira kwa vijana nchini na kulinda afya zao  pamoja na kutengeneza mawasiliano  ya wadau hivyo Bima Marathon wana lengo hilo kwa watoto njiti.

Amesema Kuna makusanyo yanayopatikana kwenye kujiandikisha kwenye hizi mbio, sehemu yake inakwenda kupelekwa kwaajili ya kufariji watoto  waliozaliwa njiti katika wodi yao maalum.

"NIC tuliona kupitia mbio hizi tushiriki kuweza kusaidia watoto hawa kwani ni jamii ambayo inatakiwa kuangalia kwa karibu”. Amesema Mwakifulefule.

Mwakifulefule ametoa wito kwa watanzania kuendelea kujiandikisha kwa kujitokeza kwa wingi waje kushiriki mbio hizo kwani kushiriki kwao si tu watakimbia na kulinda afya zao lakini pia watasaidia watoto njiti waweze kufanikisha ndoto zao

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bima Marathon Baraka Mtavangu amewashukuru NIC kwa kuweza kuwa wadhamini wao katika mbio hizo hivyo wamekuwa na mchango mkubwa hasa katika kuleta tabasamu kwa watoto njiti ambao ni Taifa la leo.

Hata hivyo amesema washiriki wote watakaoshiri watepewa tshirt na medali pamoja na mshindi wa kwanza atapewa milioni moja, mshindi wa pili atapewa laki saba na mshindi wa tatu atapewa laki tano hii ikimaanisha kwamba washindi wa kiume na washindi wa kike tuti ya kilometa 10 na kilometa 21.

“Katika kilometa 5 zawadi zote ambazo tumeziweka kwa mshindi wa kwanza atapewa laki mbili, mshindi wa pili laki moja na mshindi wa tatu 50,000 hii ni kwa watoto ambao watakuwa wamekuja kukimbia ama kutembea kwenye kilometa tano”. Amesema Mtavangu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...