***********************************

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo na Waziri wa Uwekezaji, Mhe. Geofrrey Mwambe kwa pamoja wamekutana leo Mei 11, 2021 na kufanya mazungumzo na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo ya Uingereza, Bw. James Duddridge.

Katika kikao hicho Mawaziri hao wamepata fursa ya kujadili masuala mbalimbali ya kudumisha na kukuza mahusiano ya biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza hususani kwa bidhaa muhimu za Tanzania kuuzwa nchini Uingereza na kuvutia  Uwekezaji mkubwa wa Uingereza hapa nchini.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu,  Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Prof. Godius Kahyarara pamoja na Balozi wa  Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...