Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wakala wa Umeme Vijijini REA na Wadau wa Umeme EDPG kutoka Norway wakati wa kikao cha pamoja leo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha pamoja baina ya REA na EPDG leo jijini Dodoma.
Mwakilishi wa EPDG akizungumza wakati wa kikao kazi cha pamoja na REA jijini Dodoma leo.
Watendaji wa Wakala wa Umeme Vijijini REA na Wadau wa Umeme EDPG kutoka Norway wakisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja Leo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha pamoja.


 Charles James, Michuzi TV

SERIKALI  imesema kufikia mwaka 2022 itakua imekamilisha mchakato wa kuweka nishati ya umeme kila Kijiji Nchi nzima na baadhi ya vitongoji.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja alipokua akifungua mkutano wa pamoja baina ya  Wakala wa Nishati Vijijini REA na Wafadhili wa mradi huo kutoka Norway, EDPG wenye lengo la kuangalia maendeleo ya miradi inayotekelezwa na Wakala huyo nchini.

Mhandisi Masanja amesema kikao hicho kinalenga kukumbushana nia ya REA kupeleka umeme kila Kijiji pa pamoja na kukagua miradi hiyo pamoja na kujadili mpango kazi wa kutekeleza miradi ya umeme Vijijini.

" Nchi yetu imepiga hatua kubwa Sana katika kusambaza umeme, ukiangalia mwaka 2015 ni vijiji takribani 2,000 pekee vilivyokua na umeme, lakini leo tunazungumzia vijiji 10400 vina umeme Kati ya 12,000 nchi nzima.

Umeme ni nyenzo muhimu katika ukuaji wa uchumi wa Nchi yetu, ukiangalia maeneo mengi yenye umeme yamepiga hatua za kimaendeleo, tunaendelea na juhudi zetu za kuhakikisha tunafikia maeneo mengi zaidi ili kuweza pia kufungua fursa za kiuchumi kwenye maeneo hayo," Amesema Mhandisi Masanja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Julius Bundala amesema tayari wameanza mzunguko wa pili wa awamu ya tatu ambapo miradi hii ya umeme vijijini kwa asilimia 90 inatekelezwa kwa fedha za serikali huku asilimia 10 pekee zikitoka kwa wafadhili.

" Kupitia kikao hiki na wadau wetu hawa tutajadili bajeti na mkakati wa kuweza kutekeleza miradi yetu na tunaamini wafadhili wetu hawa watatusaidia kutekeleza miradi hii kwenye baaedhi ya maeneo.

Hadi kufikia Desemba 2022 vijiji vyetu vyote nchini vitakua vinawaka umeme na sasa tutakua na kazi ya kuanza kuwasha umeme kwenye kila kitongoji, lengo letu ni kuifanya Tanzania yenye umeme wa kutosha ili tuweze pia kuchochea ukuaji wa uchumi wetu," Amesema Bundala.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Wateja wa REA, John Zolotu ametoa rai kwa wateja wote wa REA kuhakikisha wanatumia mafundi wanaotambulika na Tanesco wakati wakufanya 'wiring' kwenye nyumba zao ili kuepuka vishoka wanaoweza kuwafanyia kwa bei kubwa.

" Sisi Kama REA hatutaki kuona mwananchi ambaye anaishi nyumba isiyo na umeme, na hiyo ndio maana tumeanza na umeme vijijini kisha vitongoji vitafuatia, rai yangu kwao ni wahakikishe wanatumia mafundi wanaotambulika pindi wanapofanya wiring kwenye nyumba zao ili kuepuka vishoka ambao wanawachaji bei kubwa," Amesema Zolotu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...