.Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Watumishi kutoka TAWA mara baada ya hafla ya utiaji saini wa kanuni za Uwekezaji wa Kimkakati katika maeneo  ya  Uhifadhi uliofanyika leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza kabla ya hafla ya utiaji saini wa Kanuni za Uwekezaji  katika maeneo ya Uhifadhi nchini ambapo amesema kanuni hizo zinamruhusu Mwekezaji kumiliki eneo la Uhifadhi kwa miaka isiyopungua miaka 25.Kamishna Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi akiwa  Kamishna Msaidizi wa Biashara na Huduma za Utalii kutoka TAWA  wakifuatilia utiani Saini wa Kanuni za Uwekezaji wa Kimkakati katika maeneo ya Uhifadhi nchini uliofanyika leo Jijini Dodoma.


WIZARA ya Maliasili na Utalii imefungua milango mipya katika Sekta ya Utalii nchini kwa kutia saini ya  Uwekezaji wa kimkakati katika  maeneo ya Uhifadhi nchini kwa Wawekezaji wenye mitaji mikubwa wa kutoka ndani na nje ya nchi. 

Ameyasema hayo leo Jijini Dodoma, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro   wakati akitia saini  kanuni za Uwekezaji wa kimkakati katika maeneo ya Uhifadhi

 nchini.

 

Waziri wa Maliasili na Utalii amesema utiaji saini huo ni miongoni mwa  njia  zitakazochangia kuongeza idadi ya Watalii kufika milion 5  na mapato yapatayo bilion 6 ifikapo mwaka 2025 kupitia Sekta ya Utalii nchini.

 

 

Kwa mujibu wa Kanuni hizo Wawekezaji wataweza kuwekeza katika maeneo ya Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu pamoja na Maeneo ya Wazi ya Wanyamapori kwa miaka isiyopungua 25.

 

Akizungumza kabla ya utiaji saini huo, Waziri Dkt.Ndumbaro amesema kanuni hizo zimelenga Wawekezaji wenye mitaji mikubwa ambao hata watalii watakaokuja katika maeneo hayo ni Watalii wenye fedha nyingi ikiwemo watu maarufu duniani.

 

Amesisitiza kuwa kanuni hizo zitawezesha Wawekezaji hao kujenga mahoteli katika maeneo ya Uhifadhi pamoja na kuweka miundombinu ya Utalii itakayosaidia kuwavutia Watalii wengi kutembelea katika maeneo hayo.

 

Awali amesema kanuni hizo ni mpya na uwekezaji huo katika maeneo hayo utakuwa wa aina yake kwa vile umelenga Wawekezaji wenye mitaji mikubwa watakaowavutia Watalii matajiri hali itakayopelekea pato la taifa kuongezeka maradufu kupitia sekta ya utalii nchini.

 

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) Meja Jenerali ( Mstaafu)  Hamis Semfuko amesema utiaji saini wa kanuni  ni moja ya hatua muhimu ya kupanua fursa zitokanazo na sekta ya utalii nchini.

 

" Tuliamua kuja na wazo hili ili Wawekezaji wenye mitaji mikubwa waweze kuwekeza katika maeneo ya Uhifadhi ambapo awali uwekezaji wa namna hii ulikuwa hauwezekani" alisisitiza Mwenyekiti huyo Meja Jenerali ( Mst) Semfuko

 

 

Kwa upande wake , Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.Allan Kijazi amesema atahakikisha Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, ( TFS ) nao wanasaini kanuni za namna hiyo nao waweze kuwavutia Wawekezaji kuwekeza katika maeneo yao kwa vile wa maeneo yenye sifa kawa yalivyo ya TAWA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...