Wasani wakitoa burudani wakati Kampuni ya Jenga Afya Tokomeza Umasikini( JATU) ilipokuwa ikiwa kwenye kampeni ya kuhamasisha wananchi kununua hisa za kampuni hiyo.
Maofisa JATU wakitoa ufafanuzi kuhusu umuhimu wa wajasiriamali kununua hisa za kampuni hiyo kwa ajili ya kujikomboa kiuchumi.

Na Mwandishi Wetu

MAMIA ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wameendelea kuhamasika kwa kuendelea kununua hisa za Kampuni ya Jenga Afya Tokomeza Umasikini( JATU) ambazo lengo lake ni kuwakomboa kiuchumi.

Kampuni ya JATU kwa sasa inaendelea na kampeni ya kuhamasisha wananchi kununua hisa kwa lengo la kujikomboa kiuchumi huku wananchi hao mbali ya kununua hisa za kampuni hiyo wamepongeza ubunifu huo.

Wakizungumza leo,mamia ya wananchi wa maeneo ya Mwenge mkoani Dar es Salaam ambapo JATU walikuwa wakiendelea na kampeni ya kuhamasisha ununuzi wa hisa hizo, wamesema kampuni hiyo imekuja wakati muafaka na kwamba wataendelea kununua hisa ili kujikomboa kiuchumi kupitia miradi ya maendeleo.

Wamesema kuwa baada ya kampeni hiyo ambayo lizinduliwa mapema wiki hii katika eneo la Bunju A jijini Dar es Salaam kwa kulenga kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kumiliki hisa za JATU kama dhamana ya kuendeleza kwa faida shughuli zao za kiuchumi, wananchi wa Mwenge nao walikuwa wakiisubiria kwa hamu kutokana na umuhimu wake katika kuwakomboa kiuchumi.

Juma Mchomola na Mwanaamina Hamisi wamesema kupitia kampeni ya JITU wamepata mtazamo mpya na fikra mpya na hasa kujiamini katika shughuli za ujasiriamali wanazozifanya na hivyo watakuza biashara wanazofanya.

Akifafanua zaidi Mwanaamina Hamisi anasema "Huu ubunifu umenifumbua macho, na umenivuta kuingia moja kwa moja katika umiliki wa hisa za JATU, nimeona unanipa urahisi mkubwa wa kudhaminika kwa kupewa mikopo mingine yenye riba au isiyo na riba,"amesema.

Dereva Bajaji wa eneo hilo la Mwenge Mtumwa Jonasi amesema  kampeni hiyo ni rafiki sana na mipango ya Serikali ya kutokomeza umasikini na kwamba watu wote wanaojihusisha na ujasiliamali, kilimo au  biashara ni wakati mwafaka kwao kujiunga na hisa za JATU.

Kwa upande wao maofisa wa JATU wamesema pamoja na mambo mengine,lengo la  kampeni ya ununuzi wa hisa za kampuni hiyo umelenga kutoa elimu kwa Watanzania kuhusu kujiamini kwenye mikakati yao ya kujikwamu kwenye umasikini.

Ameongeza hisa moja ya  JATU inauzwa Sh.500 tu, na mwananchi ili kujiunga anatakiwa kununua hisa 10, ikiwa na maana ya Sh. 5,000 na kila mwisho wa mwaka anapata gawio kwa faida ikizingatiwa hisa za kampuni yao zipo kwenye soko la hisa la Dar es Salaam.

Aidha uwekezaji wa kampuni hiyo upo katika kilimo cha kisasa cha mashamba makubwa ya nafaka, matunda pamoja na biashara mbalimbali za mazao katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...