Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KATIKA kuhitimisha wiki ya Utumishi wa Umma siku ya Jumatano tarehe 23 Juni, 2021, Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imejipanga kutoa mafunzo kwa kundi maalumu la Wanahabari Wanawake wa Dar es Salaam.
Mafunzo
hayo yanalengo la kuwajengea uwezo Wanahabari hao juu ya masuala
mbalimbali ya fani ya Ununuzi na Ugavi yatakayofanyika katika ukumbi wa
PSSSF Golden Jubilee Tower jijini Dar es salaam.
Akizungumza
na Michuzi Blog kwa niaba ya Uongozi wa PSPTB, Mkuu wa kitengo Cha
Masoko na Uhusiano kwa Umma, Bi Shamim Mdee amesema kuwa milango ipo
wazi kwa Watu, Mshirika, Wazabuni au Taasisi mbalimbali kupata ushauri
wa kitaaluma katika Bodi hiyo, kwani ni moja ya majukumu yao.
Amesema
mafunzo kama haya yamekuwa yakitolewa kwa Taasisi mbalimbali za Umma na
binafsi suala ambalo limesaidia taasisi nyingi za umma kupata hati Safi
na kupunguza kama sio kuondoka kabisa baadhi ya changamoto zilizokuwa
zinawakabili.
“Hali hii itasaidia Wanahabari kubobea katika kuandika na kuripoti kwa ufanisi habari za Ununuzi na Ugavi”, amesema Shamim.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...