Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wakati Tanzania ikiwa kwenye uchumi wa kati unaotegemea zaidi viwanda,serikali mkoani Njombe imewataka maofisa biashara kutanua wigo  wa kibiashara   pamoja na kuondoa urasimu wakati wa utoaji huduma katika jamii.

Kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe,mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri wakati wa kufunga mafunzo ya siku tano ya sheria ya leseni za biashara chini ya wakala wa usajili wa biashara na leseni (BRELA) amesema ni muhimu maofisa biashara wote nchini kuondoa urasimu wa kufanya makadirio ya biashara kwa kuwakomoa wananchi pamoja na kuongeza wigo wa kutafuta fursa zaidi badala ya kujifungia ofisini.

“Mimi naomba tukajitafakari zaidi,hawa wanaoanzisha biashara tuwalee na tuwathamini pamoja na kuwaelimisha kwasababu biashara inahitaji zaidi elimu”alisema Ruth Msafiri

Awali afisa leseni kutoka BRELA  Bi,Saada Kilabula alisema wameendelea kufanya majadiliano ya sheria za biashara ili kuweka mazingira rafiki kwa kila anayefanya biashara kwa maslahi mapana ya uchumi wao na taifa kwa ujumla.

“Katika kutekeleza majukumu mara nyingi kuna kuwa kuna mkanganyiko ndio maana tumeanzisha haya mafunzo kwa kuanzia kwenye hii kanda ili wote twende kwa pamoja na tutoke na lugha moja tunamshukuru Mungu kwa siku hizi tano tuliyoyafanya ni makubwa”alisema Saada Kilabula

Baada ya mafunzo hayo yaliyohusisha maofisa kutoka mikoa mitatu ya Njombe,Iringa na Ruvuma baadhi ya maofisa biashara akiwemo Cassim Mohamed kutoka Mafinga na Upendo Mwankemwa kutoka halmashauri ya mji wa Njombe wamesema wanaamini sheria na mafunzo waliyoyapata yatakwenda kuwasaidia katika kuwaelimisha wafanyabiashara kwani wengi wao wamekuwa wakikaidi kukata leseni kutokana na uelewa mdogo katika suala la kufuata sheria katika biashara zao.

Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri kwa niamba ya mkuu wa mkoa huo, akifunga mafunzo kwa maafisa biashara wa mikoa mitatu katika semina ya siku tano iliyokuwa ikiendeswa na maafisa leseni kutoka BRELA huku akiagiza maafisa hao kupunguza urasimu.
Baadhi ya maafisa biashara wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi wakati wakifunga semina yao ya siku tano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...