Na Karama Kenyunko Michuzi TV
SERIKALI imesema katika kumtambua mtoto inaweka msisitizo katika kwa jamii kutambua umuhimu wa mtoto kulindwa ili kuzuia vitendo vya ukatili dhidi yao.

Imesema mtoto ana haki ya kulindwa na mtu yoyote kwani kutakuwa na kizazi chenye upendo na endelevu.

Akizungumza katika tamasha la Siku ya Mtoto wa Afrika lililoandaliwa na Taasisi ya WLAC, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Stella Msophe amesema serikali imefanya jitihada mbalimbali za kumlinda mtoto ikiwemo kutunga sheria ya mtoto ya mwaka 2009.

Amesema sheria hiyo imetokana na sera ya mtoto ya mwaka 2008 na kwamba lengo ni kuhakikisha mtoto anatambuliwa, kulindwa na kupatiwa haki zake zote za msingi.

Amesema jamii inapaswa kuhakikisha inamlinda mtoto na kumpatia haki zake ikiwemo elimu, afya na malazi.

"Ukatili unaofanywa kwa watoto asilimia kubwa hutokana na familia hivyo, tuwalinde watoto wetu. Mtoto hapaswi kubaguliwa," amesema Zombe.

Naye, Ofisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Kinondoni, Agnes Mbusa amesema wamekuwa wakipokea mashauri ya kulawiti na wazazi wamekuwa wakipewa rushwa na wahalifu.

Amesema mashauri yanapelekwa polisi na mahakamani lakini baadae mzazi na muhalifu wanatafutana na kuingia makubaliano ya kupeana fedha.

"Wazazi kuahidiwa kupewa Shilingi laki tatu au mbili na inawezekana mtoto kama mwanafunzi anahamishiwa shule ili kufuta ushahidi. Hata afisini mwetu kunaletwa mashauri na wakati tunaendelea kuwasikiliza mzazi mmoja anajitokeza na kusema wamefikia makubaliano hii ni changamoto kubwa,"

Amesema kwenye ofisi za ustawi kuna mashauri mengi ya ukatili wa kingono, watoto kutekelezwa na wengine kukataliwa na kwamba jitihada zao zimewasaidia kuwafanya watoto wengi kusaidiwa.

Amesema ni jukumu kwa wazazi kuwalinda watoto wao kwani kupokea fedha kutoka kwa wahalifu bado hakuondoi mtoto kudhalilika.

Amesema jamii isaidie kuibua uovu unaofanywa kwa watoto kwa kuripoti matukio hayo ustawi wa jamii.

"Watoto wakulinde wenyewe, wasipokee zawadi wala kupanda lifti kutoka kwa watu ambao hawawafahamu." Amesema

Kwa upande wake, Ofisa wa Polisi kutoka Dawati la Jinsia na Watoto Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lea Mbunda amesema wanaendelea kuelimisha jamii kuhusu ukatili kwa watoto na asilimia kubwa wazazi ndio wanaochangia.

Amesema ulinzi wa watoto unaanzia nyumbani na kwamba watoto wengi wanafanyiwa ukatili kutokana na ukaribu wa ndugu wanaowaona na kuwaamini.

Pia amesema kutengana kwa wazazi kumekuwa changamoto kwa watoto kusababishwa vitendo vya ukatili.

" Hakuna ushirikiano kati ya wazazi hawafiki kutoa ushahidi mahakamani na sababu ni kukubaliana kinyumbani ili kuepuka adhabu. Wazazi mkumbuke athari zinazowapata sasa hazitafutika hadi ukubwani kwani machangudoa na wezi huanzia hapo." Amesema Mbunda.
Mwalimu Esther Romani wa shule ya msingi Mburahati akiwa katika picha na mwanafunzi wake, Ibrahim Mohamed sharifu ambaye ni ,mshindi wa kwanza wa mashindano ya kuchora katika shule kumi, akifirahia zawadi zake na tuzo wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyoandaliwa na kituo cha Msaada wa Sheri kwa wanawake, WLAC Juni 18,2021 jijini Dar es Dalaam.
Mrakibu wa polisi, kutoka Dawati la Jinsia na Watoto Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lea Mbunda, akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika yaliyofanyika Viwanja vya TTCL Kijitonyama jijini Dar es Salaam, yaliyoandaliwa na WLAC.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Stella Zombe akizungumza katika tamasha la  Siku ya Mtoto wa Afrika lililoandaliwa na WLAC, Juni 19, 2021 jijini Dar es Salaam
Wakili Abia Richard kutoka kituo cha sheria cha msaada kwa wanawake WLAC, akionesha picha za kupinga ukatili wa kijinsia zilizochorwa na wanafunzi kutoka shule mbali mbali za Msingi kwa wageni waliohudhuria siku ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Jijini Dar es Salaam


Picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...