Mapokezi ya Klabu ya Simba mkoani Ruvuma wakiwasubiri Azam FC katika mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Majimaji mkoani humo June 26, 2021.
Kikosi cha Yanga SC kikitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Tabora wakiwafuata Biashara United mchezo wa Nusu Fainali ya ASFC utakaopigwa kwenye dimba la Ali Hassan Mwinyi June 25, 2021.
Kikosi cha Azam FC kikioanda Ndege kuwafuata Simba SC katika Nusu Fainali ya Michuano hiyo utakaopigwa kwenye dimba la Majimaji mkoani Ruvuma.

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV 

MABINGWA Watetezi wa Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC), Simba SC wametua mjini Songea mkoani Ruvuma tayari kwa mchezo wao wa Nusu Fainali ya Michuano hiyo dhidi ya Azam FC mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Majimaji June 26, 2021.

Simba SC watamenyana na Azam FC katika mchezo huo wakati Young Africans wenyewe wakicheza na Biashara United ya Mara mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora, June 25, 2021 siku ya Ijumaa.

Kuelekea michezo hiyo, Simba SC na Young Africans wamevunja rekodi katika mapokezi yao baada ya kutua kwenye Mikoa hiyo, Simba SC (Songea) na Yanga SC (Tabora) wakati Azam FC wao wakielekea kimya kimya Songea kuwakabili Simba SC.

Wanajeshi wa Mpakani, Biashara United haijafahamika kama wametua Tabora au la! bali wamewataka mashabiki wao kujitokea kwa wingi katika dimba hilo la Ali Hassan Mwinyi ili kuwaangamiza Wananchi katika mchezo huo.

Simba SC wamefuzu hatua ya Nusu Fainali ya Michuano hiyo baada ya ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC mchezo uliopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, wakati Young Africans wenyewe wakipata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Mwadui FC mchezo uliochezwa kwenye dimba la CCM Kambarage, Shinyanga.

Biashara United walifika hatua hiyo walipopata ushindi wa bao 2-0 dhidi Namungo FC mchezo uliopigwa kwenye dimba la Kumbukumbu ya Karumbe mkoani Mara, Azam FC walifuzu Nusu Fainali kwa ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la CCM Kambarage, Shinyanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...