TAKWIMU zinaonesha takribani watu 10 kati ya 100 wana tatizo la ugonjwa wa Kisukari ambapo asilimia 60 ya wagonjwa wa ugonjwa huo hawajui kama wanaumwa.

Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt.James Kihologwe wakati akizungumza kwenye mkutano wa Waganga Wakuu na   Waratibu wa Magonjwa yasiyoambukiza ambao walitoka katika  Mikoa 26.

Dkt.Kihologwe amesema  magonjwa ambayo yakuambukiza yamekuwa yakiongezeka nchini na takwimu zinaonesha kwamba watu  26 kati ya 100 wanamatatizo ya shinikizo la juu la damu.

Amesema takribani watu 10 kati ya 100 au asilimia 9 wanatatizo kubwa ka Kisukari ambapo amedai pamoja na ukubwa huu lakini takwimu zinatuonesha kwamba takribani asilimia 60 ya  wagonjwa huo hawajijui kwamba wana tatizo la Kisukari.

Pia amesema  watu 36 mpaka 22 wanamafuta mengi katika mishipa yao ya damu ambapo amedai zaidi ya robo tatu ya watu wenye shinikizo la juu la damu hajijui kama wana tatizo hilo.

“Lakini zaidi ya robo tatu ya watu wenye shinikizo la juu la damu hawajijui kama wanatatizo hilo unasikia tu mtu amenguka hajijui,”amesema.

Mkurugenzi huyo Msaidizi amesema matatizo hayo yamekuwa yakiongezeka kwa watanzania hivyo kupunguza maendeleo ya Nchi ambapo amedai katika kila asilimia 10 ya ongezeko la magonjwa hayo yamekuwa  yakipunguza pato kwa asilimia 0.5.

“Tunasema katika kila asilimia 10 ya ongezeko la magonjwa haya linapunguza pato la Nchi kwani  asilimia 0.5 na maana yake ni kwamba tutakuwa hatuna nguvu kazi ya kutosha katika maendeleo  pamoja na gharama kubwa ya matibabu kwa wagonjwa,”amesema.

Amesema kutokana na ongezeko la magonjwa ambavyo sio ya kuambukiza,Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imekuja na mpango wa kuhakikisha matitizo hayo yanapungua kwa kuja na mpango wa kubadili mtindo wa maisha ili kukabiliana na  magonjwa  yasiyoambukiza.

Akifunga  mkutano huo,Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe,amesema Nchi imekuwa na mipango mikakati mingi ambapo amedai mingi imekuwa haiwasaidii watanzania.

Aidha,amewataka waratibu wa afya katika mikoa kusimamia zoezi la kupambana na magonjwa yasiyokuwa yakuambukiza.

“Lakini nilitaarifiwa kwamba mmepewa adidu za rejea sisi tutahakikisha tunapata ripoti kutoka katika mikoa juu ya utekelezaji wa masuala ya magonjwa ambayo sio ya kuambukiza.

“Hii tungependa iende sambamba na upatikanaji  wa takwimu sahihi kwani huwezi kuchukua hatua ni lazima watu wawe wanapima uzito kila inapobidi na lazima tuanzishe Club za michezo katika Hospitali za rufaa za Mikoa.Ndio maana humu ndani tuna waganga wakuu na warataribu,”amesema.

Amesema kwenye upande wa Lishe Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imefanikiwa kwani Mikoa imeandikishana mikataba ya utendaji kazi na Waziri wa Tamisemi ambaye alikuwa akifanya kwa niaba ya Rais.

Amesema lazima wataalamu hao  watoe elimu kuhusu jinsi ya kula milo  kwani wengi wamekuwa wakipotoshwa.

“Kwa sasa  tuna miongozo kama sita wa kwanza ni usimamizi wa vituo vya kutolea huduma kwa kutumia kamati kwenye ngazi wa kituo,mpango wa maendeleo wa afya ya msingi awamu ya pili,”amesema.

Naye,Katibu Mkuu Chama cha Ugonjwa wa Kisukari Prof.Kaushik Ramaiya,amesema magonjwa manne ambayo yamekuwa ni hatari  kwa sasa ni Sukari,Moyo,Mapafu na Saratani.

Amesema ili kukabiliana na magonjwa hayo ni lazima watu wafanye mazoezi ambapo amedai zaidi ya asilimia 80 ya magonjwa ambayo sio ya kuambukiza  yanaweza kuzuilika.

Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Magonjwa yasiyoambukiza Dkt.James Kihologwe akizungumza wakati wa Mkutano wa Waratibu wa Magonjwa yasiyoambukiza kwa ngazi ya Mikoa 26 iliyoshiriki uliofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Chama cha Ugonjwa wa Kisukari Prof.Ramaiya,akielezea umuhimu wa mafunzo kwa washiriki wakati wa Mkutano wa Waratibu wa Magonjwa yasiyoambukiza kwa ngazi ya Mikoa 26 iliyoshiriki uliofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe,akimkabidhi Kitabu cha Muongozo wa Mtindo wa Maisha na Magonjwa Yasiyoambukiza Mwaandishi wa habari wa Fullshangwe Blog.Bw.Alex Sonna baada ya  Mkutano wa Waratibu wa Magonjwa yasiyoambukiza kwa ngazi ya Mikoa 26 iliyoshiriki uliofanyika jijini Dodoma.
Meneja Mpango wa Taifa wa Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa yasiyoambukiza Dkt.Omary Ubuhuyu ,akizungumza kwenye Mkutano wa Waratibu wa Magonjwa yasiyoambukiza kwa ngazi ya Mikoa 26 iliyoshiriki uliofanyika jijini Dodoma.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Best Magoma,akizungumza kwenye Mkutano wa Waratibu wa Magonjwa yasiyoambukiza kwa ngazi ya Mikoa 26 iliyoshiriki uliofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe,akimkabidhi Kitabu cha Muongozo wa Mtindo wa Maisha na Magonjwa Yasiyoambukiza Mwaandishi wa habari wa Fullshangwe Blog.Bw.Alex Sonna baada ya  Mkutano wa Waratibu wa Magonjwa yasiyoambukiza kwa ngazi ya Mikoa 26 iliyoshiriki uliofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe,(hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa Waratibu wa Magonjwa yasiyoambukiza kwa ngazi ya Mikoa 26 iliyoshiriki uliofanyika jijini Dodoma.

 Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe,akiwa katika picha za pamoja na washiriki mara baada ya kufunga  Mkutano wa Waratibu wa Magonjwa yasiyoambukiza kwa ngazi ya Mikoa 26 iliyoshiriki uliofanyika jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...