- yaingizwa kwenye mradi mkubwa wa kukuza Utalii Afrika

Na Mwandishi Wetu, Windhoek, Namibia.

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii [UNWTO], kupitia mkutano wa siku tatu wa kujadili nchi za Afrika jinsi gani zitajikwamua kutokana na madhara ya janga la UVIKO 19 na Utalii unaofanyika mjini hapa, limeikubalia Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano ujao wa masuala ya Utalii Bara la Afrika ambapo pia wameiingiza Tanzania kuwa nchi ya tatu itakayowezeshwa mradi mkubwa wa masuala ya Utalii.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Damasi Ndumbaro ambapo amebainisha kuwa, Ujumbe wa Tanzania umeweza kupata faida hizo mbalimbali  sambamba na kupata uzoefu mkubwa ikiwemo pia kutangaza fursa za Utalii za Tanzania katika mkutano huo ambao una wadau wakubwa wa Utalii.

"Tumekutana nchi nyingi za Kiafrika, tumejadili mambo mengi, tumebadilishana uzoefu mkubwa tumepata mawasilisho mbalimbali kutoka kwenye makampuni yenye uwezo wa juu kabisa wa kutangaza utalii duniani.

Lakini pia tumepata fursa ya kufanya mikutano ya ana kwa ana na wadau mbalimbali moja kati ya wadau hao ni Katibu Mkuu ambaye anayeshughulikia masuala yaUtalii wa Umoja wa Mataifa Bw. Pololikashvili, ambaye amekubali mkutano ujao wa Utalii Barani Afrika, ufanyikie Tanzania". Alisema Mhe. Dkt. Ndumbaro.

Mhe. Dkt. Ndumbaro ameongeza kuwa, Katibu huyo pia amekubali yeye mwenyewe binafsi kutembelea Tanzania na kuonana na viongozi mbalimbali wa Kitaifa pamoja na wadau wa utalii kwa ajili ya kufanya maongezi juu ya mustakabali wa Utalii baada ya UVIKO 19.

Ambapo pia amesema wameweza kuomba na kukubaliwa kuiingiza Tanzania kuwa  moja kati ya nchi tatu Barani Afrika ambazo zitapata mradi wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya Utalii.

"Nchi zingine zikiwa Namibia na Cape Vede ambazo zimeshaingizwa toka zamani kwa namna ya kipekee Tanzania tumepewa upendeleo huo baada ya kushiriki hapa na tayari tutaingizwa katika mradi huo mkubwa…". Alisema Mhe. Dkt. Ndumbaro.

Aidha, amesema Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo umepata utaalam na uzoefu mkubwa kwa jinsi gani watakavyoweza kunasuka na ugonjwa huo wa UVIKO 19, amewapongeza watanzania kushiriki na kuweza kufanikiwa.

Katika mkutano huo, leo 16 Juni unatarajiwa  pia Rais wa Namibia atashiriki kuufunga huku Mawaziri 15 kutoka nchi 15  za Afrika ikiwemo Tanzania kupata nafasi ya kuziongelea nchi zao katika mkutano ambao utarushwa moja kwa moja na televisheni mbalimbali za ndani na nje ya Namibia ikiwemo mitandao ya Kijamii.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia) akimkabidhi zawadi mbalimbali kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)  Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii (UNWTO) Zurab Pololikashvili (kushoto)  mara baada  kufanya kikao cha ana kwa ana kando ya mkutano huo wa  Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akipeana mkono na Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii (UNWTO), Zurab Pololikashvili mara baada  kufanya kikao cha ana kwa ana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia) akifanya kikao cha ana kwa ana na Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii (UNWTO) Zurab Pololikashvili (kushoto)  mara baada Mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika hilo.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...