Na Amiri Kilagalila,Njombe


Jumuiya ya umoja wa wanawake UWT ccm wilaya ya Njombe imesema imefanikiwa kuongeza kiwango cha makusanyo katika vyanzo vyake toka milioni 94 kwa kipindi kilichopita hadi zaidi ya shilingi milioni 100 kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na viongozi pamoja na wanachama wake.

Katika kikao cha baraza la jumuiya hiyo katibu wa UWT wilaya ya Njombe Sauda Mohamed katika taarifa yake amesema fedha hizo zinapatikana kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali vya mapato ikiwemo ukodishwaji wa vibanda vya biashara pamoja na ubinifu wa vyanzo vipya vya mapato.

“Jumla ya mapato yetu kwa mwaka mzima ni milioni mia moja laki tano na arobaini na awali jumuiya ilikuwa inakusanya mapato milioni tisini na nne kwa sasa imeongezeka”alisema Sauda

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Njombe Beatrice Malekela amesema sera yao ya kuwawezesha wanawake ili waondokane na utegemezi imeanza kufanyiwa katika katika kata mbalimbali wilayani humo.

“Sera ya CCM ni pamoja na kuhakikisha wanawake wanajiunga na vikundi vya wajasiriamali kwa hiyo tulipopota kweye kata ndani ya majimbo yote tumeona namna wanawake wanavyoendelea kuunga mkono juhudi za kujiwezesha kiuchumi”alisemaBeatrece Malekela

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Njombe Pindi Chana katika kikao hicho cha baraza amesema ni muhimu kuendelea kushikamana katika shughuli mbalimbali ikiwemo kuungana katika kuviwezesha vikundi mbalimbali hatua ambayo itawasaidia kusonga mbele.

Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe Skolastika Kevela licha ya kupongeza jitihada kubwa zinazofanywa na jumuiya hiyo wilaya lakini ameonesha kusikitishwa na uhai wa wanachama kwani wengi wao wanashindwa kulipa ada jambo ambalo linakwamisha jitihada za chama na jumuiya yenyewe.

Betrece Malekela mwenyekiti wa UWT wilaya ya Njombe akiendelea kuhamasisha wanawake wa wilaya hiyo kuendelea kuimarisha uchumi wa chama,jumuiya mtu mmoja mmoja ili kufikia mafanikio.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...