Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Joyce Ndalichako kesho Juni 21, 2021 anatarajia kufungua Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Sekondari (UMISSETA) kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Mashindano haya yanajumuisha mikoa yote kutoka Tanzania Bara na Visiwani ambapo yatafanyika kwenye viwanja vya Nangwanda Sijaona, Chuo cha Walimu Mtwara (TTC kawaida) Chuo cha Walimu Ufundi maarufu kama Mwasandube, na viwanja vya Shule ya Sekondari ya Ufundi Mtwara ambapo yanaanza kesho Juni 21, 2021 na kumalizika Julai 03, 2021. Mashindano yameandaliwa na Wizara tatu zinazohusika na Elimu, Michezo na TAMISEMI chini ya Kamati ya Uratibu ya Kitaifa ya Makatibu Wakuu wa Wizara hizo.

Mashindano haya yalitanguliwa na Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa Juni 8, mwaka huu mjini Mtwara na kufungwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Pauline Gekul Juni 18, 2021.

Michezo itakayoshindaniwa katika mashindano haya ni mpira wa miguu kwa wasichana na wavulana, mpira wa miguu maalum kwa wavulana (wenye ulemavu wa kusikia) mpira wa pete, mpira wa wavu kwa wasichana na wavulana, mpira wa mikono kwa wasichana na wavulana, mpira wa kikapu kwa wasichana na wavulana, mpira wa meza kwa wasichana na wavulana, riadha jumuishi, kwaya na ngoma.

Aidha, kutakuwa na mashindano ya usafi katika mazingira wanayoishi. Mashindano yatapambwa na wasanii mbalimbali wa kizazi kipya wakiongozwa na Mauwa Sama na Chege ili kutoa hamasa na burudani. Pia vyama vya michezo, mashirikisho na vilabu vya michezo mbalimbali vimealikwa kuja kuangalia vipaji mbalimbali.

Kauli mbiu ya michezo ya mwaka huu ni “Michezo, Sanaa na Taaluma kwa Maendeleo ya Uchumi wa Viwanda”

Imetolewa na

John Mapepele
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...