WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya China Railway 15 Bureau Group Corporation ya China inayojenga barabara ya kutoka Ruangwa hadi Nanganga na kuwataka waongeze kasi ili waweze kukamilisha kwa wakati.
 
Ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Julai 26, 2021) alipokutana na viongozi hao katika kijiji cha Namahema  wilayani Ruangwa. Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 53.2 inatarajiwa kugharimu kiasi cha sh bilioni 59.28 na imepangwa kukamilika Novemba 2022.
 
Mheshimiwa Majaliwa amesema barabara ya Ruangwa - Nanganga ni muhimu kwani kukamilika kwake kutarahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo yakiwemo mazao mbalimbali ya kilimo hivyo kuchangia katika kukuza uchumi na kuongeza tija kwa wakulima.
 
Kwa upande wake, Meneja Mkaazi wa kampuni ya China Railway 15 Bureau Group Corporation Bi Su Jinlan amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba wataongeza kasi ya ujenzi wa mradi wa barabara hiyo na kwamba itakamilika kwa wakati. Hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 18 ya utekelezaji.
 
Meneja huyo amesema kuwa kampuni yao imejipanga ipasavyo na wanatarajia kuongeza vifaa vya kufanyia kazi ili waweze kukamilisha ujenzi mradi kama ilivyokusudiwa. Pia amewashukuru wananchi wa wilaya hiyo kwa ushirikiano wanaoutoa kwao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...