Mkuu wa Jeshi la Nchini (IGP) Simon Sirro akizungumza kuhusiana na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi Polisi kuingia katika Uwakala wa Bima katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi Polisi (TPFCS ) Toyi Ruvumbagu akizungumza kuhusiana na utekelezaji wataofanya katika kuhudumia Jeshi hilo katika Bima .
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Dk.Elirehema Doriye akizungumza kuhusiana na utendaji wa Shirika katika kuwafikishia watanzania huduma za Bima zilizo katika hafla ya kuingia makubaliano Kati NIC na Jeshi la Polisi.

*NIC yaahidi kuendelea kutoa huduma bora za Bima
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amelitaka Shirika la Bima la Taifa (NIC) kuhakikisha linatoa elimu ya kutosha kwa jeshi la polisi kuhusu umuhimu wa kuwa na bima za maisha ili kuwezesha askari wengi kujiunga na huduma hiyo kwa maana wapo kwenye kazi hatarishi katika kazi zao.

Akizungumza katika hafla ya Kuandikishiana Hati ya Makubaliano hafla ya Kuandikishina hati ya makubaliano kati ya Shirika la Taifa la Bima(NIC ) na jeshi la polisi kupitia Shirika la Uzalishaji mali la Jeshi hilo ya kuwa Wakala wa Bima iliyofanyika Makao makuu ya shirika hilo Jijini Dar es salaam IGP Sirro amesema kuna ulazima wa shirika la bima la NIC kutanua wigo na kuweza kuwafikia watanzania wengi waweze kupata uelewa wa huduma za bima na kuweza kujiunga na huduma hiyo kwani inamanufaa makubwa pia ni Shirika la watanzania.

"Vijana wetu wamekuwa wakigongwa na magari katika kazi zao za kupitisha magali barabarani, unamsimaisha dereva amelewa aangalii huyu ni askari polisi anamgonga kwahiyo kuwa na bima ya maisha ni jambo la msingi sana kwani wanakuwa wanafamilia zao zinazowategemea" Amesema IGP Sirro.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dk. Elirehema Doriye amesema Shirika linatoa huduma zote za bima za maisha na bima za mali na ajali, kwa kutoa huduma hizo pia inafanya huduma za uwakala wa shirika la uzalishaji mali la jeshi la polisi kuwa na wigo mpana zaidi kwa kuwafikia askari ndani ya jeshi.

"Kupitia uwakala utawezesha jeshi la polisi,maafisa,wafanyakazi pamoja na familia zao na watanzania wote kupata huduma zote za kibima kupitia wakala washirika la uzalishaji mali la jeshi la polisi". Amesema Dk.Doriye.

Pamoja na hayo Dk.Doriye amesema kupitia mahusiano yao na Shirika la uzalishaji mali la jeshi la polisi watakuwa wanaenda kutekeleza mpango mkakati wa maendeleo ya sekta ya bima ambao kwa kiasi kikubwa utaongeza ufahamu wa bima lakini pia utumiaji wa huduma za bima nchini.

"Kwa sasa utimiaji wa huduma za bima ni asilimia 15 na kwa watanzania na ili tufike mpango wa serikali ambapo kufikia mwaka 2030 asilimia 50 ya watanzania wawe wanatumia huduma za bima lakini pia uelewa wa bima kwa tanzania ni chini yya asiliia 40 na mpango wa serikali ni kuhakikisha kwamba inapofika mwaka 2030 asilimia 80 ya watanzania wanaelimu sahihi ya bima". Amesema

Hata hivyo amesema kuwa kupitia mahusiano hayo wanaenda kutekeleza pia mikakati ya serikali kuhakikisha kwamba kuna ukuaji kwenye sekta ya fedha.

Nae Makamu Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Uzalishaji Mali ya Jeshi la Polisi (TPFCS) Toyi Ruvumbagu amesema kupitia makubaliano hayo jeshi litanufaika na fursa kama kupata wepesi wa kufikia huduma za bima kwa askari nchini, kumbukumbu zinaonesha kwamba idadi ya askari na maofisa wa jeshi la polisi wanaopata huduma za bima hasa bima ya maisha iko chini hivyo kupitia fursa hii ya shirika linakusudia kutumia mifumo ya kijeshi kuhamasisha askari kujiunga na huduma hii

Aidha amesema jeshi la polisi litanufaika kwa kuweza kupata bei za kimakundi kwa bima ya afya ambayo ni group cover na kulingana na idadi ya ya askari na maofisa watakaojiunga na bima hiyo ambao zinaunafuu ukilinganisha na bei za kawaida za soko.

"Kwa mfano tukipata kuunga askari mmoja mpaka askari elfu 10, tutapata punguzo la asilimia Tano tukiweza kupata askari elfu 10 mpaka shilingi 20,000 tutapata punguzo la asilimia 7.5 tukipata askari elfu 20 mpaka wakafika askari 30 tutapata punguzo la asilimia 10% kutoka bima yeu hii na tukipata askari zaidi ya elfu 30 tutapata punguzo la asilimia 12 ". Amesema Bw.Ruvumbagu.

Amesema kupitia fursa hiyo kutawezesha askari wetu kujiunga katika huduma kwa bei rafiki iwapo kundi kubwa litahamasika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...