Na Mwandishi Wetu, Dar  Es Salaam.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)  Shaka Hamdu Shaka amesema Tanzania hakuna mapambano ya demokrasia kwani mageuzi na mabadiliko toka  mfumo wa Chmaa kimoja na kuingia vyama  vingi yamefanyika kwa ridhaa na kwa mujibu wa sheria kinyume na madai yaliyotolewa na katibu  mkuu  wa chadema John Mnyika.

Shaka ametoa kauli hiyo leo Julai 31,2021 baada ya Mnyika ,ambapo amesema madai  ya kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman ametekwa na polisi wakati polisi  si watekaji bali ni walinzi wa amani, usalama wa raia na mali zao na wajibu wanaoutekeleza kwa mujibu wa katiba na sheria.

Shaka amesema wamemsikia John Mnyika akidai Tanzania iko kwenye mapambano ya demokrasia ambapo alisema si ajabu na wala si kosa kwa Polisi kumkamata kiongozi yeyote  wa kisiasa au wa kiserikali  ikiwa wataona kuna haja ya kufanya hivyo.

"Kinachofanywa na CHADEMA ni kutapatapa, na kuuhadaa umma wa watanzania na jumuiya za kimataifa ilhali masuala ya ndani ya nchi kwa mujibu  wa sheria hufanyika pale inapobidi na mamlaka za utawala hazihitaji kibali toka jumuiya  zozote za nje au za ndani.

"Jumuiya za kimataifa zikiwemo  taasisi zinazoshughulikia haki za binadamu ,demokrasia na utawala bora zina taratibu na  mipaka  zinapotaka kujua yanayoendelea au kujiri  katika taifa  fulani  hivyo hazina haki ya kuziamuru mamlaka zilizopo kisheria ili zifuate  matakwa yao.

"Polisi  wamethibitisha kumkamata Mbowe  na wala hajatekwa kama Mnyika na chadema wanavyodai. Matamshi yao yamelenga kujenga chuki na kuchafua taswira ya nchi yetu kwenye Jumuiya ya kimataifa jambo ambalo halikubaliki na hawatafanikiwa maana Tanzania ni nchi huru inayoongozwa kwa misingi ya utawala wa sheria,"amesema Shaka.

Amesisitiza si kweli kwa mujibu wa  matamshi ya Mnyika  kudai Tanzania iko katika mapambano ya demokrasia wakati demokrasia ipo  kisheria na kikatiba zaidi Tanzania ni nchi ya kupigiwa mfano katika kuzingatia ustawi wa haki  za binadamu na maendeleo ya demokrasia.

Amemmtaka Mnyika awe na uwezo wa kutofautisha nini maana ya ukandamizaji  wa demokrasia na uhuru wa demokrasia kutumika isivyo na kusababisha  uvunjaji na ukiukaji wa sheria za nchi.

"Kutumia kivuli cha demokrasia kuvunja sheria huko ni kuinajisi demokrasia  kwani moja ya misingi muhimu ya demokrasia ni utawala wa sheria. Hivyo haya wanayoendelea nayo ni upotoshaji na propaganda za kitoto. Vyama vyote vya vya siasa vimesajiliwa kwa mujibu wa sheria hivyo vina wajibu wa lazima kuwa mfano kwa kutii na kutekeleza sheria za Nchi."amesema.

Aidha amewataka  viongozi wa CHADEMA  kukaa na kutafakari kwa busara, hekima na uwazi kwanini Mbowe amepewa mashtaka hayo na kupitia wanasheria wao wakajiridhisha juu ya hatua sahihi za kuchukua badala ya kueneza proganda ambazo hazitamsaidia au kuzuia taratibu za kisheria kuendelea dhidi yake. Haya wanayoyafanya ni muendelezo wao wa kutokupenda kuheshimu na kufuata utaratibu.

"Ikiwa hati ya mashitaka iliyowasilishwa mahakamani iko kinyume na sheria mwenye uhalali wa kisheria kueleza vinginevyo ni mahakama tu si yeyote. Sasa kama wao wanahisi kuna jambo halipo sawa wafuate taratibu za kisheria kupata tafsiri wanayoona wanaistahili badala ya kutaka kulazimisha uvunjwaji wa katiba na sheria za nchi.

Katika hili niwakumbushe chadema moja ya misingi muhimu ya demokrasia ya kweli ni pamoja na kuheshimu na kutekeleza kwa usawa utawala wa sheria. Ikiwa wanaiishi demokrasia na wanaitaka ionekane ikiishi ni vyema wakaheshimu utawala wa sheria ambao hakuna mtu yupo juu ya sheria.

Kukamatwa kwa kiongozi yeyote aidha wa Chama tawala au wa upinzani si shambulio dhidi ya demokrasia kama anavyodai mnyika huku ajijaribu kumshinikiza  Rais Samia Suluhu Hassan amuamuru mwendesha mashitaka amuachie huru mbowe kitu ambacho ni kinyume kabisa na matakwa ya kisheria.

Shaka amesema  ni kituko kukisiskia chama kinachohubiri kufuata misingi ya utawala bora wa sheria huku kikishindwa kuheshimu mgawanyo wa madaraka na kutaka kuingilia uhuru wa mahakama.

"Mnataka demokrasia, utawala wa sheria na haki, halafu muda huo huo mnamtaka Rais aingilie mahakama akiuke katiba na Sheria za Nchi kwa Maslahi yenu hili halikubaliki kabisa. Serikali ya  Rais Samia itasimamia katiba, sheria, haki na usawa wakati wote bila kuyumba wala haya kwani kufanya hivyo ndio chachu ya amani na utulivu nchini." Shaka

Katibu  wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...