Na Khadija Seif,Michuzi TV

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameendelea kuwaamini wanawake kwa kuwateua na kuwapa nafasi mbalimbali kwenye Serikali yake ya Awamu ya Sita.

Agosti 2 mwaka huu, Rais ametangaza wakurugenzi ambao watakwenda kutumikia majukumu yao kwenye halmashauri mbalimbali na katika uteuzi huo wanawake wameendelea kupewa nafasi ya kuaminiwa na Rais.

Miongoni mwa wanawake ambao wamepata nafasi ya kuaminiwa na Rais Samia na kuteuliwa kushika nafasi ya Ukurugenzi wa Halmashauri basi ni pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Hanan Mohammed Bafagil.

Awali katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe katika nafasi ya Ukurugenzi alikuwa Mussa Gama ambaye sasa amehamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbuka mkoani Ruvuma.Hanan kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha Mkoa wa Arusha.

Akizungumza leo Agosti 3,2021, na Michuzi TV na Michuzi Blog Hanan amesema anatoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassa kwa kumuani na kumteua kwenye nafasi hiyo,hivyo atahakikisha anafanya kazi kwa bidii na maarifa yake yote ili kuonesha imani yake kwa Rais na Watanzania hususan wananchi wa Wilaya ya Kisarawe.

"Kuteuliwa kwangu na Rais kwenye nafasi hii , ninachoweza kwanza namshukuru Rais kwa imani yake kwangu lakini nieleze huu ni mwendelezo tu wa kuendelea kupiga kazi , nimetoa Arusha na sasa nimehamia Wilaya ya Kisarawe hakuna kulala nitaendelea kuungana na wananchi kuhakikisha maendeleo katika wilaya yanapatikana,"amesema .

Aidha amewaomba wananchi wa Wilaya hiyo kuonyesha ushirikiano katika kila namna huku yeye akiahidi kuwa atashirikiana na wananchi pamoja wakuu wote wa idara katika kufanikisha azma ya Serikali ya kupeleka maendeleo kwa wananchi inatekelezwa kwa kasi.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kisarawe Mkoa wa pwani Hanan Mohammed Bafagil

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...