Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame mara baada ya kuwasili katika eneo la Uwekezaji wa kiwanda cha Inyange Plant Entrance kilichopo mjini Kigali Rwanda leo Agosti 03,2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na mwenyeji wake Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakiangalia baadhi ya Bidhaa mbalimbali zinazozalishwa katika kiwanda cha Inyange Plant mjini Kigali wakati walipotembelea kiwanda hicho leo tarehe 03 Agosti,2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia moja ya aina ya simu zinazotengenezwa katika kiwanda cha Mara Phone Mjini Kigali Rwanda, wakati alipokua katika ziara yake ya siku ya pili nchini Rwanda leo tarehe 03 Agosti,2021. Kulia ni Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rwanda baada ya kukamilisha ziara yake ya siku mbili Nchini Rwanda leo tarehe 03 Agosti,2021.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...