Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Phillip Mpango (kulia) akiwa na mke wake Mama Jenisia Mpango  wakipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Nd. Theobald Sabi kuhusu mikakati ya benki hiyo katika  kukopesha wajasiriamali wadogo alipotembelea banda la benki hiyi kwenye maonyesho ya tatu ya SIDO yaliyofanyika Mjini Kasulu Mkoani Kigoma.


BENKI ya Taifa ya Biashara imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo kwa njia mbali mbali zikiwemo kuunda akaunti zisizo na gharama za uendeshaji, kuwapa mafunzo yanayolenga kuwaongezea ujuzi zao pamoja na kutoa mikopo yenye masharti na riba nafuu. 

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi wakati akizungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Phillip Mpango wakati wa ufunguzi rasmi wa Maonyesho ya Tatu ya Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) yanayofanyika kitaifa Mjini Kasulu Mkoani Kigoma.

“Benki ya NBC imekuwa ikotoa elimu kwa wajasiriamali kupitia semina mbali mbali za mafunzo zinazotolewa kwenye kliniki za NBC Biashara Club kwa kushirikiana na SIDO na TanTrade. Mafunzo hayo yanawalenga wajasiriamali kutoka sekta mbali mbali zikiwema biashara, kilimo, madini na nyingine nyingi.,”

Akdha, Sabi amesema Zaidi ya mafunzo ya usimamizi fedha na biashara, wajasiriamali hao pia huelekezwa namna ya kupata huduma katika Benki ya NBC hususan mikopo na akaunti za gharama nafuu, kutengeneza mpango wa biashara ili kumuwezesha mjasiriamali  kuendesha biashara katika namna inayomfanya ajue kama anapata faida au hasara. 

Akiongea na Makamu wa Rais, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC. Theobal Sabi alibainisha kwamba benki hiyo tayari imeshatoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya TSHs 10B kwa Mkoa wa Kigoma na kwamba zaidi ya kutoa mikopo pia inafuatilia kwa ukaribu miradi na wafanyabiashara na kutoa elimu na ushauri.

“Tuna makubalianona SIDO pamoja na TanTrade kuhahakikisha kwamba tunaendelea kuwasaidia wajasiriamali na wazalishaji wadogo wadogo kwa dhamira ya kuunga mkono jihudi za serikali katika kukuza uchumi na kuongeza ajira. Kwa hapa Mkoa wa Kigoma benki yetu ya  NBC imeshatoa mikopo jumla TSHs 10B na tunaendelea kushirikiana na Vyama vya Ushirika (AMCOS) mbali mbali kuhakikisha fedha tunazotoa zinawafikia hata wale walio katika sekta ya kilimo.” Alisema  Theobald Sabi.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Phillip Mpango alitaka ufafanuzi zaidi wa mazingira ya ukopeshaji wa benki hiyo hususan kwenye masuala ya riba,  masharti ya ya ukopeshaji na kama wakopaji wanaongezeka na changamoto zao.

Akiendelea kutoa maelezo kwa Makamu wa Rais, Mkurugenzi Mtendaji alisema kwamba wakopaji wanaongezeka na ni kutokana na jitihada za benki hiyo za kulegeza masharti, kutoa mikopo kwa riba nafuu ya isiyozidi 16% pamoja na kushirikiana na wadau wengine wakiwemo Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB.)

Makamu wa Rais, Dkt. Phillip Mpango alitoa matumaini yake ya siku zijazo kwenye swala la riba na kuitaka benki hiyo kuhakikisha kwamba riba inashuka zaidi hususan kwa wakina mama ambao kwa uzoefu ni walipaji wazuri wa mikopo.

“Tumaini langu kwa NBC ni kwamba riba ishuke na hasa kwa vikundi vya wajasiriamali na wakina mama kwa sababu ni walipaji wazuri. Muangalie na vyombo vingine ambavyo vinaweza kugusa wenye mahitaji zaidi, mkalijadili kwenye Tanzania Bankers Association namna gani mnateremsha riba. Nataka kuona tofauti ili Watanzania wa hali ya chini waweze kukopa kwenye mabenki yetu, hasa haya ya kizalendo.” Alisema Makamu wa Rais, Dkt. Phillip Mpango.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Sabi alipokea maelekezo na changamoto kutoka kwa Makamu wa Rais, Dkt. Phillip Mpango na kumuhakikishia  kwamba tayari benki hiyo imeliangalia swala la riba na tayari wapo wateja ambao ni walipaji wazuri wananufaika na punguzo la riba na kwamba juhudi hizo hazitaishia hapo. 

Maonyesho hayo ya Tatu ya SIDO yamewaleta pamoja wadau mbali mbali wakiwemo wajasiriamali, taasisi za kifedha kama Benki ya NBC akiwa mdhamini mkuu, asasi na mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na uongozi wa Serikali katika ngazi tofauti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...