Na Karama Kenyunko -Michuzi TV

MAHAKAMA Kuu Divisheni ya Uhujumu uchumi na makosa ya Rushwa maarufu Mahakama ya  Mafisadi imewataka mawakili wa upande wa utetezi katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watatu kuacha kuwauliza mashahidi maswali ya dhihaka na kejeli na badala yake waulize maswali kwa  kuzingatia utu wa shaidi na kwa mujibu wa utaratibu

Jaji Mustapha Siyani ametoa maelekezo hayo leo Septemba 17,2021 wakati Wakili wa utetezi Peter Kibatala akimuhoji Shaidi wa pili wa upande wa Jamuhuri , Inspekta Mahita Omari Mahita baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na wenzake watatu

Maelekezo hayo yamekuja baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi Pius Hilla kudai kuwa kila wakili wa utetetezi Peter Kibatala anapomaliza kuuliza swali anatoa neno la unyanyasaji kwa shaidi jambo ambalo si sahihi na kumlazimu  kuiomba mahakama kutolea uamuzi suala hilo.

"Nakubaliana na hoja ya Hilla ni kweli wakati wa kuuliza maswali kama ambavyo mnasema mtuhumiwa akikamatwa wazingatie utu na nyie zingatieni utu wakati wa kumuhoji shaidi", amesema Jaji Siyani

Mapema Wakili Kibatala alimuuliza Shaidi hivi "unajua kwamba uko hapa mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi katika kesi ndogo dhidi ya kesi ya msingi".Shahidi  akajibu kuwa hafahamu ndipo Kibatala akasema kumbe wako na shahidi ambaye hata haelewi nini kimempeleka mahakamani, jambo lililosababisha waliouwa ukumbi wa mahakama kucheka.

Awali, wakati shahidi wa kwanza wa upande wa Jamuhuri, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Ramadhani Kingai akitoa ushahidi wake alitaka kutoa maelezo ya onyo ya mshtakiwa Adam Kasekwa kama kielelezo lakini upande wa mashtaka ukiongozwa na Kibatala walipinga maelezo hayo kupokelewa wakidai kuwa mshtakiwa huyo wakati akichukuliwa maelezo pia maelezo yake yalichukuliwa nje ya muda.

Mapingamizi hayo yalisababisha kusimama kwa kesi ya msingi ya tuhuma za ugaidi na kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo ndogo ndani ya kesi ya msingi

Mapema, akitoa ushaidi wake, Shahidi Mahita amedai katika hatua nzima ya ukamatwaji wa washtakiwa hao hakuna mahali popote ambapo washtakiwa waliteswa  kabla ama wakati wa kuchukuliwa  maelezo yao  ya Onyo kama ambavyo upande wa utetezi unadai.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Pius Hilla  shahidi  Mahita amedai, katika kipindi hicho washtakiwa walipata huduma zote wanazostahili kupewa binadamu ikiwemo kupatiwa chakula

Amedai Agost 4, 2020 majira ya Saa 11 jioni alipigiwa simu  na ACP  Ramadhani Kingai alimwambia aende kwake  na alipofika alimweleza kuwa kuna kazi ya kufanya.

 Amedai kuwa Kamanda Kingai alimwambia awaandae askari  ambao ni ACP Jumanne Gudluck na  Francis na Dereva Azizi ambapo baadae walikwenda Moshi ambapo mbali na mambo mengine walielekezwa kuwa kuna kikundi cha watu ambacho kimepanga kufanya matukio ya ugaidi katika maeneo mbalimbali ya Nchi ikiwa ni pamoja na Dar es Salaam,  Mwanza, na Arusha.

 Pia alielezwa kuwa kikundi hicho kilipanga kumdhuru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Olesabaya, hivyo wanatakiwa kuwakamata kabla ya kufanya uhalifu huo.

 Amedai baada ya kupewa malekezo walianza safari kwenda Moshi ambapo katika upelelezi wao na kwa kutukia wasiri wao walifanikiwa kuwamata washtakiwa a Adam Kasekwa na Mohamed Lingwenywa  eneo la Rau Madukani  Moshi mjini.

Amedai, baada ya kuwapekua washtakiwa wao walikutwa wakiwa na silaha moja na kete za dawa za kulevya aina ya heroin.Baada ya taratibu mbalimbali za upelelezi walielekezwa kuwasafirisha watuhumiwa Dar es Salaam.
 
 Kingai alidai sababu za kuwapeleka Watuhumiwa  hao Dar  es Salaam ni kutokanana Kuwa kesi ya hiyo imefunguliwa katika Jiji hilo. Amedai baada ya kufika Dar, waliwahifadhi washtakiwa katika kituo cha cha polisi cha Central na baadae kuwahamishia katika kituo cha polisi Mbweni kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na kutoharibu upelelezi.

Akijibu maswali  ya upande wa utetezi kwa nini waliwatoa washtakiwa katika kituo cha polisi cha Central na kuwapeleka kituo cha Mbweni,  Inspekta Mahita amesema, waliwahamishia watuhumiwa hao Mbweni kwasababu kituo hicho hakina muingiliano wa watu wengi, pia ni  kituo cha ufuatiliaji.

Ameendelea kudai lengo lingine la kuwapeleka kituo hicho cha Mbweni ilikuwa ni kuwaweka washtakiwa hao kila mmoja kwenye chumba chake ili wasiharibu upelelezi na pia washtakiwa hao ni Makomandoo. Washtakiwa wote katika kesi hiyo ni, Freeman Mbowe, Halfan Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Abdallah Ling'wenya.

Mashashtaka yanayowakabili watuhumiwa katika kesi ya msingi ni pamoja na  kula njama za kutenda ugaidi ambapo Mbowe anatuhumiwa kufadhili vitendo hivyo vya kulipua vituo vya mafuta kwa kutoa zaidi ya Sh.600,000.

Inadaiwa Mbowe alituma kiasi hicho cha fedha kwa washitakiwa wenzake kwa ajili ya kufanya maandalizi ya vitendo vya ugaidi ikiwemo kutaka kulipua vituo vya mafuta, mikusanyiko ya watu, kukata miti na kuisambaza barabarani.

Piaa watuhumiwa wote wanatuhumiwa kushiriki vikao vya kutenda kosa la ugaidi huku mshtakiwa wa pili anatuhumiwa kumiliki bastola yenye risasi tatu kwa ajili ya kutenda kosa la ugaidi. Aidha, mshtakiwa wa kwanza anatuhumiwa kumiliki nguo, begi na koti zote za Jeshi la Wananchi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...