Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Poland na Klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani, Robert Lewandowski ametangazwa kutwaa Tuzo ya Mfungaji bora wa Ulaya na kutwaa zawadi ya Kiatu cha Dhahabu akifunga mabao 41 katika Ligi Kuu Soka nchini Ujerumani (Bundesliga) msimu uliopita wa 2020-2021.

Lewandowski anashikilia rekodi ya aliyekuwa Mshambuliaji wa Kimataifa wa Ujerumani Magharibi na Klabu hiyo, marehemu Gerd Müller ambaye alifanya hivyo kutwaa zawadi kama hiyo kati ya mwaka 1970 na 1972, Pia aliweka rekodi ya kufunga mabao 365 katika michezo 427 katika historia yake ya soka barani Ulaya.

Kupitia Tovuti ya Bayern Munich, Lewandowski aliyetajwa kuwa na mabao 284 katika michezo 355, amenukuliwa akisema, “Napenda kuishukuru familia yangu, Wachezaji wenzangu, Makocha na Benchi lote la Ufundi na wengine wote. Nisingeweza kushinda zawadi hii bila wao. Katika michezo, kama kwenye maisha, kila mmoja ni muhimu sana, pia najaribu kuwa mfano kwa wengine. Na hii ni kwa nini? ndio maana naipeleka zawadi hii kwa kila mmoja ambaye yupo na mimi kila siku. Nafurahi kila tukipata mafanikio pamoja kama timu. Ahsanteni sana”.

Rais wa Bayern Munich, Herbert Hainer amesema hayo ni mafanikio makubwa kwa Lewandowski yanayotokana na uhodari wake katika soka, mafanikio hayo yanampa kila kitu na kupata kile anachostahili kila siku. Lewandowski amestahili kutwaa Tuzo hii ya Mfungaji bora akiwa wa pili tangu kufanya hivyo kwa Mshambuliaji Gerd Müller.

Afisa Mtendaji Mkuu na Golikipa wa zamani wa Klabu hiyo ya Bayern, Oliver Kahn ameeleza kuwa Nyota huyo ameweka historia katika Klabu hiyo ya Bayern, kwa wenzake na kwake binafsi, “Lewandowski ni mfano wa wengine ameonesha jinsi gani ni Mchezaji wa Kimataifa akiwa hapa Bayern, ametumia muda mrefu hapa na ameshinda mataji mengi”.

Mjumbe wa Bodi wa Klabu ya Bayern Munich, Hasan Salihamidzic amesema Tuzo hiyo inawapa furaha na nguvu kama Viongozi wa Klabu katika kuiongoza timu hiyo. Salihamidzic amesema wanajivunia Lewandowski katika timu hiyo sambamba na kuwapa changamoto wengine wanaotaka kupata mafanikio kama yeye.

Tuzo ya Kiatu cha Dhahabu barani Ulaya inatolewa na Vyombo vya Habari vya Michezo barani humo kila mwaka kwa Mfungaji bora kila msimu. Akiwemo Gerd Müller, kuna Wachezaji wengi wamewahi kuzawadiwa tuzo hiyo, wakiwemo Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, Francesco Totti, Thierry Henry, Ronaldo, Marco van Basten, Hristo Stoichkov na Eusebio. Waliowahi kuwa Wachezaji wa Bayern Munich, Roy Makaay na Luca Toni ni miongoni mwa Wachezaji waliotwaa tuzo hiyo, wakicheza timu za Deportivo La Coruna na Fiorentina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...