Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiongozana na mkewe Bi. Mbonimpaye Mpango hii leo Septemba 23,2021 wameshiriki Ibada ya Misa takatifu ya nadhiri za kwanza na za daima kwa masista 12 wa kanisa katoliki, ibada iliofanyika katika kanisa la mtakatifu Marco Mwinjili Parokia ya Kabanga wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Ibada hiyo imeongozwa na mhashamu baba Askofu Joseph Mlola wa Jimbo katoliki Kigoma ambapo Masista hao wanajiunga shirika la moyo safi wa Maria (Bene-Maria).

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ibada hiyo, Makamu wa Rais amewasihi viongozi wa dini k kuendelea kuliombea taifa kwani ili kufukia maendeleo ya haraka pamoja na mambo mengine ni muhimu taifa kuwa na amani. Amesema ni wajibu kwa viongozi wa dini kuendelea kuwakumbusha waumini katika kufanya kazi kwa bidii kama ilivyoandikwa katika maandiko matakatifu.

Aidha Makamu wa Rais amewaasa wale waliofunga nadhiri hizo kuwaombea viongozi wa taifa ili wafanye kazi kwa kuwatumikia wananchi na si vinginevyo. Amesema ni muhimu kwa wazazi kuendelea kutoa malezi bora kwa watoto wao ili kuwa na kizazi chenye kujali Amani na matendo mema.









 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...