Na Mwamvua Mwinyi,Kisarawe
MKUU wa Mkoa wa Pwani Aboubakar Kunenge ameweka bayana changamoto kubwa inayomnyima usingizi mkoani Pwani ,ni migogoro ya ardhi ambapo ameelekeza mabaraza ya ardhi yawe jibu la kutatua changamoto hii kwa kutenda haki.

Amesisitiza mabaraza hayo kusimamia pia sheria, kwa kusikiliza pande zote za mgogoro na kuepuka mgongano wa maslahi katika kushughulikia migogoro ya ardhi.

Msisitizo huo aliutoa wakati akiwaapisha wajumbe wa Baraza la ardhi la Wilaya ya Kisarawe .

Alisema kuwa lengo la Serikali ni kusogeza huduma karibu na Wananchi hivyo baraza la hilo la kisarawe limeundwa ili kutimiza azma hiyo.

"Wilaya ya Kisarawe hapo awali haikuwa na Baraza la Ardhi, Wananchi walilazimika kwenda Wilaya ya Kibaha pindi wanapopata Migogoro ya Ardhi, sasa wasaidieni.” Alisema Kunenge.

Mkuu huyo wa mkoa pia aliwafunda wajumbe hao kuacha kutekeleza majukumu yao kwa kudai rushwa akisema “hawa wananchi ambao wanakuja kwenye Baraza la Ardhi hawana fedha, wengine wamevamiwa ardhi yao na watu wenye uwezo wa kifedha, tuwasaidie Wananchi wetu kupata haki yao.”

Kunenge aliwaeleza wajumbe hao kuwa kitendo cha kuwaapisha maana yake pia ni kuwa atawafuatilia utendaji kazi wao na akawahimiza Viongozi na Watendaji wa Serikali kuhakikisha kuwa kesi zinapungua na zikifika kwenye Mabaraza kesi hizo ziishe mapema kwasababu ya ushahidi mzuri kutoka kwa Watendaji na Viongozi wa Serikali.

Kuhusu Mabaraza ambayo hayafanyi kazi, Mkuu huyo wa Mkoa amemuagiza Katibu Tawala Mkoa kufuatilia na kuhakikisha kuwa Mabaraza ya Ardhi ya kata ambayo hayafanyi kazi yanafanyiwa utaratibu wa kisheria ili yafanye kazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...