Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imetoa Siku Saba kwa Maafisa Utumishi wa Halmashauri zote Nchini kuhakikisha wanapeleka orodha ya majina ya watumishi wanaodai malimbikizo ya mishahara yao ili waweze kulipwa stahiki zao.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi wakati akizungumza na watumishi wa Jiji la Arusha ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuzungumza na kutatua changamoto za watumishi wa umma nchini.

Akiwa katika mkutano na watumishi hao Moja ya malalamiko aliyoyapata ni ya watumishi kutolipwa malimbikizo ya mishahara yao kwa muda mrefu, ambapo Naibu Waziri Ndejembi amesema changamoto haipo wizarani wala Hazina ambapo ndio hulipa bali uzoefu unaonesha maafisa utumishi ndio wamekua wakichelewesha kupeleka majina ya watumishi wao wanaodai.

"Hii changamoto tunakutana nayo karibia kila Halmashauri ya watumishi kulalamika kucheleweshewa kulipwa madeni yao, lakini niwahakikishie shida haipo kwetu Wizarani wala Hazina shida iko kwa Maafisa Utumishi hawa ndio huchelewesha kuleta majina ya watumishi wanaodai, sasa natoa siku saba hadi kufikia Ijumaa majina yawe Wizarani.

Idara za Utumishi kwenye Halmashauri zipitie madeni yote ya watumishi na yaletwe kwetu ili tuweze kuyasukuma Hazina watu walipwe haki zao, madeni haya siyo hisani ni mishahara na haki yao pengine walishindwa kupata kwa sababu ya kuchelewa kurekebisha daraja lilivyopanda lakini ni haki yao, asitokee mtu akaona wanafanyiwa hisani, Leteni majina yao tuwalipe wote," Amesema Ndejembi.

Ametoa wito kwa Watumishi wa Jiji la Arusha na Halmashauri zingine ambao wanadai kuonana na Maafisa Utumishi wao ili kuhakikisha majina yao yanawekwa kwenye orodha ambayo itatumwa Wizarani.

Naibu Waziri Ndejembi pia amesisitiza mahusiano mazuri makazini huku pia akiwataka watumishi wa umma kuheshimu mamlaka na kutii maagizo yanayotolewa na viongozi wao.

" Kuna changamoto kubwa ya mahusiano kwenye hizi Halmashauri zetu na hasa kwenye Majiji makubwa, unakuta Mkuu wa Idara hamheshimu Mkurugenzi  na Mkurugenzi hamheshimu Mkuu wa Wilaya, niwatake kuheshimu Mamlaka siyo DC anatoa maagizo wewe unafanya yako," Amesema Ndejembi.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ndejembi amekutana na kuzungumza na Maafisa na Askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ambapo amewasisitiza kufanya kazi kwa weledi, nidhamu na kuweka mbele maslahi ya Taifa.

 

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Sophia Mjema.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Sophia Mjema akizungumza katika kikao cha pamoja cha Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora na Watumishi wa Jiji la Arusha.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi akizungumza na Maafisa na Askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...