Na.Vero Ignatus,Arusha

Zaidi ya Asasi 161 Jijini Arusha zimeshiriki katika maonyesho ya kwanza kufanyika, yakiwa na lengo la kuonyesha kazi mbalimbali wanazozifanya katika jamii,pamoja na kubadilishana uzoefu na kuangalia changamoto mbalimbali katika utendaji kazi

Akizungumza Msajili msaidizi wa Masaidizi wa NGO Jiji la Arusha Fatuma Amir ,alisema kuwa mashirika 91 yanafanya kazi ndani ya  jiji la Arusha ambapo 70 zinafanya kazi nje ya jiji, wanasema wamekuwa wakikutana kila kwenye vikao vya robo kama inavyotakiwa ili kuboresha utendaji kazi pamoja na kuangalia marekebisho mbalimbali yanayohitajika.

Ametaja changamoto kubwa ni npamoja ya baadhi ya wadau kutekeleza shughuli zao bila kutoa taarifa sambamba na kutokuhudhuria vikao vya robo kama inavyostahili ili kuboresha utendaji kazi katika utendaji wao

Mgeni  rasmi katika maonyesho hayo Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha  Athuman Kihamia ,aliwataka Wakurugenzi wa Ngo hizo kufanya kazi kwa kuzingatia sheria,kanuni na taratibu haswa katika matumizi sahihi ya fedha.

Aidha Kihamia alisema kuwa asilimia kubwa wanaoendehs taasisi hizo ni wanawake ambapo kiuhalisia wanawake wengi ni wa adilifu kuliko wanaume ,hivyo wanawake wakiwezeshwa kutakuwa na Taifa la watu ambao ni waadilifu na waaminifu

‘’Ukiweza kuziunganisha Taasisi hizi kwa pamoja itasaidia kondoa changamoto zilizopo katika Jamii,kwani Asasi hizi zinaunga mkono juhudi za Serikali katika utendaji.alisema Kihamia

Alizipongeza Asasi hizo na kuwataka kutokukata tamaa,bali waendelee kujitolea na kutumia muda wao vizuri katika kuitumikia jamii,katika kutoa Elimu,Afya pamoja na namna ya kuisaidia jamii kujikwamua kiuchumi.

Aidha alisisitiza wananchi kwenda kupata  chanjo  kwaajili ya kujikinga na covid 19 pia liwataka kuchukua tahadhari kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalam wa Afya kwani Ugonjwa huo upo na unaua.

Jiji la Arusha likioatiwa chanjo 50,000 hadi  60% tayari imetumika hivyo nawasihi mjitokeze kupata chanjo,msisikilize maneno ya kwenye mtandao hii ni kwa manufaa ya Afya yako.alisema Kihamia.

Kwa upande wake mshiriki wa maonyesho hayao Mwalim William Sanin’go anayejihushisha na watoto wenye changamoto ya  ulemavu wa akili kutoka shule ya Jaffary amesema kuwa maonyesho hay ani mazuri kwani yameweza kuwaleta washiriki pamoja na kufahamiana kwa karibu

Saning’o ametoa  wito kwa jamii  kwa ujumla kwamba  pindi wanapopata wasaa na kuona maonyesho kama hayo, wajitokeze kwa wingi ili waweze kupata elimu ambayo itawasaidia wao pamoja na wale amabao wanawazunguka ,kama ujuavyo kazi kubwa ya NGO ni kutoa elimu na kuibua mambo yaliyojificha katika jamaii na kutafuta utatuzi.

Nae Nishaeli Frank kutoka Taasisi ya The Dare women’s Foundation amesema kuwa kumekuwa na mwamko mdogo kwajamii katika sehemu ambayo maonyesho yapo ili waje kujifunza kwani wapo nwatu wengi wenye changamoto mbalimbali kwani wengi wao wangeweza kupata utatuzi wa changamoto zao.

Inaonekana matangazo hayajafanyika vya kutosha hivyo jamii haijapata taarifa,nashauri kipindi kingine matangazo yatolewe ya kutosha ili jamii ielewe na ije kujifunza na kuona yale mambo amabayo tunayafanya katika jamii.Alisema Frank.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Athuman Kihamia akizungumza na washiriki katika maonyesho ya kwanza ya Asasi za Kiraia kuonyeshwa kazi mbalimbali wanazozifanya katika jamiii
Msajili msaidizi wa Masaidizi wa NGO Jiji la Arusha Fatuma Amir ,akizungumza na washiriki katika maonyesho ya kwanza ya Asasi za Kiraia kuonyeshwa kazi mbalimbali wanazozifanya katika jamiii
Mshiriki wa maonyesho hayo  (wa kwanza kulia )Nishaeli Frank kutoka Taasisi ya The Dare women’s Foundation akionyesha moja ya kazi za kutengeneza sodo kwaajili ya mabinti waliopo kwenye mazingira magumu.
Mshiriki wa maonyesho ya kwanza ya Asasi za Kiraia  Mwalim William Sanin’go anayejihushisha na watoto wenye changamoto ya  ulemavu wa akili kutoka shule ya Jaffary Jijini Arusha
  Joshua Mbwambo (aliyeshika kipaza sauti)kutoka Taasisi ya Vuka Initiative akitoa ufafanuzi kwa Katibu Tawala wa Mkoa Athuman Kihamia namna  Taasisi hiyo inavyojikita kupambana na  Ukatili na Unyanyasaji wa Kijinsia katika Jamii ,Wanawake na Watoto.
Baadhi ya Washiriki wa maonyesho hayo ya Asasi za Kiraia wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa Athuman Kihamia
Maonyesho ya Asasi za Kiraia yakiendelea katika viwanja vya Makumbusho Jijini Arusha

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...