Aunda kikosi kazi kuhakiki kila mkazi, mwenye kiwanja/shamba kujitokeza mbele kamati kuhakikiwa.

Aipa kamati siku 30 ambapo kila mtaa kamati itafanya kazi siku 5 mitaa 5 siku 25.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa maelekezo 8 ya kumaliza Migogoro ya Ardhi eneo la Mabwepande Kufuatia eneo hilo kuwa kinara wa Migogoro ya Ardhi Jambo linalohatarisha usalama.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo Leo wakati wa mkutano Maalumu na wakazi wa eneo hilo ambapo miongoni mwa maelekezo hayo nane ni pamoja na:-

Kuunda timu ya Wataalamu ikijumuisha Vyombo vya ulinzi na usalama, idara ya Ardhi na Wanasheria ambapo itafanya uhakiki wa nyaraka za umiliki wa Ardhi kwa muda wa siku 30.

Kukamata Watu wote waliohusika kuuza na kutapeli Wananchi maeneo ikihusisha Wauzaji, Madalali na Wenyeviti wa Mitaa waliohusika kwenye udanganyifu.

Ameelekeza Manispaa ya Kinondoni kutoa elimu ya Urasimishaji wa Ardhi kwa Wananchi.

Kufutwa usajili kwa kampuni zote za Upimaji na Urasimishaji wa Ardhi zitakazofanya kazi kinyume na taratibu.

Wenye Mashamba, Mapori, Taasisi za Umma Kuyaendeleza maeneo wanayomiliki.

Wakati Kamati unafanya kazi ni marufuku Ujenzi kufanyika pasipo kibali.

Kuainishwa kwa Maeneo yote ya Huduma za Jamii na yalindwe yasivamiwe.

Kamati kukutana na Wenye Mashamba/ Mapori ambayo maeneo yao yamevamiwa ili Kuangalia njia nzuri ya busara ya kumaliza Mgogoro ikiwemo wavamizi kukubali kumlipa mmiliki halali kidogokidogo kulingana na makubaliano yao.

RC Makalla amesema anaamini njia hiyo itakuwa Suluhu ya kumaliza Migogoro Mabwepande kwakuwa Serikali itajua wakazi halali wa eneo hilo na Kusisitiza kuwa baada ya Mgogoro kumalizika hataki kuona Mapori Mabwepande.

Aidha RC Makalla ameelekeza kusimama kwa operesheni zote za kubomoa nyumba za Wananchi mpaka hapo timu ya Wataalamu itakapomaliza kazi yake.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mabwepande,Muhajirina Kassim amemwahidi Mkuu wa Mkoa Kushirikiana na kamati aliyo iunda ili kumaliza kero za wananchinwa kata hiyo.

Kassim amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kufika kwwenye kata hiyi na kusiliza kero za wananchi.

Nae Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbopo,Mohamed Bushir amempongeza RC Makalla kwa wamuzi wake wa kuhamasisha maendeo na kutatuwa kero mabalimbali za wanachi wa mtaa huo.Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Amos Makalla kushoto akizungumza na wakazi wa kata ya Mabwepande katika mkutano Maalumu wa kutatua migogoro ya Ardhi leo jijini Dar es salaam,ambapo ametoa maelekezo Nane (8) ya kumaliza Migogoro ya Ardhi.Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Godwin Gondwe akizungumzana wananchi wa kata ya Kata ya MabwepandeKata ya Mabwepande katika mkutano Maalumu wa kutatua migogoro ya Ardhi leo jijini Dar es salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)Diwani wa Kata ya Mabwepande wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam,Muhajirina Kassim akizungumza na kutoa shukrani kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Amos Makalla kwa kutoa maelekezo Nane (8) ya kumaliza Migogoro ya Ardhi eneo la Mabwepande Kufuatia eneo hilo kuwa kinara wa Migogoro ya Ardhi Jambo linalohatarisha usalama.Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbopo kata ya Mabwepande wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,Mohamed Bushir akizungumza na Michuzi TV ameahidi kushirikiana na kamati iliyoudwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Amos Makalla ili kuhakikisha anamaliza Migogoro ya Ardhi eneo lote la Mbopo.Baadhi ya wananchi wakiandika kero zao.(Picha na Emmanul Massaka wa Michuzi TV)



Wananchi wakimsiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Amos Makalla hayupo pichani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...