- Ataka Wafiwa wapewe mwili wakazike.

-Awaonya wanaokiuka Maelekezo na Tamko la Wizara.

- Ataka Maiti kuheshimiwa.

- Awaelekeza Waganga Wakuu wa Wilaya kuhakikisha upatikanaji wa dawa muhimu za Wazee.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amepiga marufuku hospitali kuzuia maiti kwa sababu mgonjwa alishindwa kulipa deni na badala yake wakabidhi mwili kwa Ndugu wa marehemu kwaajili ya kuzika wakati taratibu nyingine zinaendelea.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo baada ya kupokea Malalamiko ya Wananchi juu ya baadhi ya hospital Mkoani humo kuendelea na utaratibu wa kuzuia maiti licha ya Serikali kupitia Wizara ya Afya kukataza uzuiaji wa maiti.

Kutoka na hilo RC Makalla amewaelekeza Waganga Wakuu wa Wilaya Chini ya Wakuu wa Wilaya kuhakikisha tatizo hilo halijirudii Katika Maeneo yao.

Aidha RC Makalla amewaelekeza Waganga Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanazingatia suala la Matibabu kwa Wazee ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa dawa muhimu kwaajili ya Wazee.

Hayo yote yamejiri wakati wa Mwendelezo wa ziara ya kusikiliza na kutatua Migogoro ya Wananchi Jimbo la Kinondoni.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...