Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) imeendelea  kung’ara kwenye maonesho ya tatu ya SIDO kitaifa kwa kuleta mashine mbili za kukamua mafuta ya mawese na alizeti.

TEMDO wamezionesha mashine hizo katika maonesho ya tatu ya SIDO yanayoendelea katika uwanja wa Umoja mjini Kasulu Mkoa wa Kigoma.

TEMDO imekuja na mashine ya kisasa ambayo inaweza kukamua mafuta ya mawese yanayotokana na zao la chikichi bila kuchemsha au kutumia maji ya moto kama ilivyozoeleka.

Afisa wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Dkt. Sigisbert Mmasi amesema Mashine hiyo inaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa wachakataji wa mafuta ya chikichi.

Dkt Mmasi amesema kuwa TEMDO ina mtambo mwingine wa kuchakata mafuta ya Alizeti kuanzia kwenye kupokea mbegu mpaka kusafisha (refinery).

Aidha, Dkt. Mmasi amesisitiza kwa  wachakataji wa mafuta ya alizeti wanunue mitambo ya kisasa inayotengenezwa na TEMDO ili waweze kusafisha mafuta kabla ya kuuza kwa walaji kwani sio salama kiafya kutumia mafuta ambayo hayaja safishwa (crude oil).

Maonesho hayo yalifunguliwa rasmi tarehe 22 septemba 2021 na Mh. Dkt. Philipo Isdory Mpango, Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na rasmi yalianza kutarehe 21 na yatafungwa rasmi tarehe 30 septemba 2021.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...