Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kamati ya Ukaguzi ya Wizara na mafunzo kwa Kamati hiyo uliofanyika jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo CPA, Christopher Nkupama
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) akionesha kitabu cha Mpango Mkakati wa Wizara na Kitabu cha Hotuba ya Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa fedha 2021/22 mara baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula (kushoto) wakati wa kikao cha uzinduzi wa Kamati ya Ukaguzi ya Wizara hiyo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula (kushoto) akimkabidhi Waziri wake Dkt. Ashatu Kijaji  kitabu cha Mpango Mkakati wa Wizara na Kitabu cha Hotuba ya Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa fedha 2021/22 wakati wa kikao cha uzinduzi wa Kamati ya Ukaguzi ya Wizara hiyo jijini Dodoma.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Ashatu Kijaji (aliyesimama mbele) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Ukaguzi ya Wizara na mafunzo kwa Kamati hiyo uliofanyika jijini Dodoma. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo CPA, Christopher Nkupama
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula (kushoto) akizungumza wakati wa kikao cha uzinduzi wa Kamati ya Ukaguzi ya Wizara na mafunzo kwa Kamati hiyo uliofanyika jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Wizarra hiyo, Dkt. Ashatu Kijaji
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula (kushoto) akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati hiyo na Menejimenti yake (hawapo pichani) wakati wa kikao cha uzinduzi wa Kamati ya Ukaguzi ya Wizara na mafunzo kwa Kamati hiyo uliofanyika jijini Dodoma.
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,
CPA, Joyce Christopher akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati hiyo na Menejimenti ya Wizara hiyo (hawapo pichani) wakati wa kikao cha uzinduzi wa Kamati ya Ukaguzi ya Wizara na mafunzo kwa Kamati hiyo kilichofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mulembwa Munaku akitoa wasilisho la Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa wajumbe wa Kamati ya Ukaguzi pamoja na Menejimenti ya Wizara hiyo wakati wa kikao cha uzinduzi wa Kamati ya Ukaguzi ya Wizara na mafunzo kwa Kamati hiyo uliofanyika jijini Dodoma
Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari CPA, Christopher Nkupama akizungumza wakati wa kikao cha uzinduzi wa Kamati hiyo kilichofanyika jijini Dodoma. Katikati ni Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Ashatu Kijaji  na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula

Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakisikiliza kwa makini wakati wa kikao cha uzinduzi wa Kamati ya Ukaguzi ya Wizara na mafunzo kwa Kamati hiyo kilichofanyika jijini Dodoma.

 

“Serikali imetupa jukumu kubwa la kuhakikisha Wizara hii inaleta mabadiliko na kuharakisha mapinduzi ya nne ya viwanda na uchumi wa dijitali kupitia Habari na TEHAMA ili tusiachwe nyuma na dunia”, hayo yamezungumzwa na  Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari akizindua Kamati ya Ukaguzi ya Wizara hiyo jijini Dodoma

Dkt. Kijaji amesema kuwa Serikali imedhamiria kuona TEHAMA inaendelea kuchangia ukuaji wa pato la Taifa na kuboresha maisha ya wananchi kiuchumi na kijamii kwa kuhuisha na kusimamia ipasavyo mifumo ya TEHAMA iliyopo na kuanzisha mifumo mipya ya usimamizi pale itakapoonekana inafaa

Amesema kuwa ni jukumu la kila mtendaji wa Wizara hiyo kuhakikisha Sekta ya Habari na TEHAMA zinasimamiwa vizuri ili kuwa na mchango chanya wa kujenga, kuimarisha na kustawisha uchumi wa nchi

Dkt. Kijaji ameizungumzia Kamati ya Ukaguzi ya Wizara aliyoizindua rasmi  leo tarehe 16 Septemba 2021 kuwa itatekeleza majukumu yake kwa kipindi cha miaka mitatu kuwa itasaidia kushauri kuhusu udhibiti na ukaguzi wa ndani ili kukidhi matarajio yanayotarajiwa kufikiwa kwa wakati na ufanisi mkubwa

Katika hatua nyingine Dkt. Kijaji ametoa rai kwa  watendaji  walio chini ya Wizara yake kufanya kazi kwa weledi, uzalendo, kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi na kutoa taarifa sahihi kwa umma ili kulinda heshima na hadhi ya nchi ya Tanzania

Akimkaribisha Waziri huyo kuzindua Kamati na Kufungua mafunzo hayo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula amesema kuwa kamati hiyo imeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2001 na kanuni zake za mwaka 2004 kama zilivyorekebishwa mwaka 2010 ambapo theluthi mbili ya wajumbe wa kamati hiyo wanatoka nje ya Wizara

Ameongeza kuwa Wizara hiyo haijawahi kupata hati chafu katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita ambayo Mwenyekiti wa Kamati hiyo CPA, Christopher Mkupama amekuwa akihudumu katika nafasi ya uenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya Wizara hiyo

Aidha, amempongeza Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara hiyo CPA, Joyce Christopher kwa ubunifu na utendaji  mzuri unaoonesha matokeo

“Wizara hii ni nyeti, wezeshi na mtambuka inayohitaji watendaji wawe na utulivu na usikivu mkubwa ili kuhakikisha malengo tuliyokabidhiwa tunayatimiza kwa kiwango cha juu”, amesema Dkt. Chaula

Dkt. Chaula amesema kuwa Kamati hiyo imepitishwa kwenye utekelezaji wa miradi inayotekelezwa na Wizara hiyo ikiwemo Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na Anwani za Makazi na Postikodi kwa lengo la kuwashirikisha kwa karibu ili kurahisisha utendaji wao wa kazi na ufuatiliaji kwa kumshauri Afisa masuuli kufanya maamuzi sahihi kwa sababu Kamati hiyo ni jicho  la Wizara litakalosaidia kuondosha hoja za ukaguzi

Amesema kuwa katika eneo ambalo Wizara hiyo imefanya vizuri ni eneo la manunuzi ambapo Kitengo cha Manunuzi cha Wizara hiyo kimeweza kusimamia  ipasavyo manunuzi na zabuni za Wizara kwa kufuata sheria na taratibu za manunuzi

Kwa Upande wa Mkaguzi wa Ndani Mkuu, CPA Joyce Christopher amesema kuwa lengo la kikao hicho mbali na uzinduzi wa  Kamati ya Ukaguzi ya Wizara hiyo ni kuwawezesha wajumbe wa Kamati hiyo kuelewa majukumu yanayotekelezwa chini ya Wizara hiyo ili wanapomshauri Afisa Masuuli wawe na uelewa wa kina wa kile ambacho wanaenda kushauri

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...