*Kiwanda kilenge ubora wa kimataifa
*KASHIMBA: Watanzania wanapatiwa ujuzi na wataalam wa
kigeni
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Katiba na Sheria imewataka wawekezaji na wafanyakazi wa kiwanda cha kimataifa
cha bidhaa za ngozi Kilimanjaro (KLICL) kufanyakazi kwa juhudi, weledi na
maarifa ili makusudio ya kuanzishwa kwa kiwanda yafikiwe.
Hayo yalisemwa Oktoba 23,
2021 na Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe.
Najma Murtaza Giga wakati wa ziara ya kamati ya kudumu ya Bunge katika kiwanda
cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro, kilichopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
“kamati itaendelea kusimamia na kushauri ili kiwanda kiwe endelevu kwa maslahi ya wananchi kwa ujumla” alisisitiza Mhe. Giga.
Mhe. Giga aliwataka watumishi wa kiwanda kuwa wabunifu na waaminifu katika kulinda miundombinu ya kiwanda ambacho ni mali ya watanzania wote.
Kwa ujumla wajumbe kamati wamepongeza
mipango ya kiwanda hicho na kushauri kilenge kuwa na viwango vya kimataifa, pia
pongezi ilitolewa kwa kutoa ajira kwa watanzania wengi ikiwemo vijana na
wanawake. kamati ilishauri elimu zaidi
itolewe juu ya bidhaa za kiwanda hicho na maduka yasambae nchi nzima.
Kwa upande wake mjumbe wa
kamati hiyo na Mbunge wa jimbo la Chonge, Mhe. Salum Saffi alishauri kiwanda
hicho kujipanga kuwa na wataalam wazawa na kuachana na tabia ya kutegemea
wageni katika uendeshaji wake.
Naye Mhe. Omary Omary
alisema, “Kwa upande wangu nimeshaanza kutumia bidhaa za kiwanda hiki, naomba
kiwanda kilengi kuzalisha bidhaa bora za
viwango ili kiweze kupata soko la uhakika, haswa kwa soko la Zanzibar”.
Mbuge wa Moshi Mjini, Mhe. Priscus
Tarimo alisema, “Wana Moshi wapo tayari kulinda kiwanda hili. Pia nashauri ili tuweze
kupata soko la uhakika la bidhaa za kiwanda hiki, tuhakikishe bidhaa zilizo
chini ya viwango haziruhusiwi kuigizwa nchini,”.
Kwa upande wake, Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshugulikia Kazi, Vijana na Ajira Bw. Patrobas Katambi alishukuru kamati hiyo
kwa kutembelea kiwanda na kusema hoja zote zimepokelewa na zitafanyiwa kazi
vyema.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Kiwanda hicho, CPA. Hosea
kashimba alisema wataalam kutoka nje waliopo kiwanda wanatoa elimu kwa
watumishi watanzania kwa kila hatua ili waweze kuendesha vilivyo kiwanda wakati
wote.
“Wataalam waliopo kiwanda wanafunga mashine mbalimbali,
tumekubaliana watumishi wa kitanzania wahusike katika kila hatua ili waweze
kupata ujuzi na hatimaye kiwanda tukiendeshe wenyewe” alisema Mwenyekiti huyo
ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa
Umma (PSSSF).
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda, Mhandisi Masud Omari
alisema kiwanda kimeanza uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za ngozi kama; viatu
vya kike na kiume, viatu vya shule na viatu vya majeshi yote nchini.
“Tumeaza uzalishaji, hivyo tunatoa wito kwa watanzania
wote kuvaa viatu vya kiwanda chetu, kwani ni bora na imara na vinapatikana kwa
bei nafuu” alisisitiza Mhandisi Omari.
Kiwanda cha bidhaa za ngozi kinamilikiwa kwa ubia kati ya
Jeshi la Magereza na PSSSF.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...