Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inawataarifu wananchi na wakazi wa Bagamoyo Mkoani Pwani hadi Kigamboni Jijini Dar es salaam kuwa, kutakuwa na upungufu wa huduma ya maji kutokana na upungufu wa maji katika Mto Ruvu.

Katika kikao na waandishi wa habari kilichofanyika leo, 23 Octoba 2021 katika makao makuu ya DAWASA, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja alisema, takwimu zilizotolewa na Wizara ya Maji kupitia Bonde la Wami Ruvu, kina cha maji cha mto Ruvu kimepungua kufuatia kiangazi cha muda mrefu.

Amesema, kufuatia upungufu wa maji mtoni, uzalishaji wa Maji umepungua kutoka lita milioni 520 kwa siku hadi kufikia lita milioni 460. Upungufu huo unatokana na kupungua kwa uzalishaji katika mtambo wa Ruvu Chini ambao husambaza maji kwa asilimia 70 ya eneo la huduma la DAWASA. Mtambo wa Ruvu Chini kwa kawaida huzalisha lita milioni 270 kwa siku na hivi sasa unazalisha kiasi cha lita milioni 210 kwa siku.

Mhandisi Luhemeja amesema DAWASA kwa kushirikiana na Ofisi za Bonde la Wami Ruvu wanaendelea na zoezi la kusitisha matumizi ya maji kwa watumiaji wengine katika mto huo ikiwa ni pamoja kusitisha vibali vya umwagiliaji ili kuruhusu maji kufika mitamboni.

Amesema, Ili kuhakikisha kuwa maji yanapatikana kwa usawa katika eneo linalohudumia na mtambo wa Ruvu Chini, DAWASA imehamisha sehemu ya maji ya Ruvu Juu ili yatumike kwa maeneo yaliyokuwa yanahudumiwa na Mtambo wa Ruvu Chini. Mabadiliko haya yanapelekea kupungua kwa msukumo wa maji kwa baadhi ya maeneo.

Amewaomba wananchi kutumia maji kwa uangalifu katika kipindi hiki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...