Na Khadija Seif, Michuzi Tv

MAKAMPUNI na Taasisi zaombwa kujitokeza Kudhamini Mashindano ya vijana hususani urembo ili kuwapa moyo na kutoa Muamko kwa waandaji wa Mashindano hayo.

Akizungumza na Michuzi Tv, Meneja Masoko wa Kinywaji chenye kilevi "Bacardi" Jason Monteiro amesema vijana Wana nafasi tofauti tofauti katika jamii lakini wakati Mwengine ni muhimu kuandaa tafrija ambazo zitaweza kujua uwezo binafsi na vipaji vya ziada vya vijana hao.

"Tunapoandaa tafrija hizo zinasaidia kuona uwezo wa vijana kama sehemu ya kipaji chake kwani ni nadra Sana kuona pasipo kuandaliwa kwa Matamasha ambayo yatamsukuma kuonyesha kipaji hiko mbele ya hadhira kutokana na kukutanishwa kwa watu mbalimbali mahala hapo."

Hata hivyo Jason ameeleza kwa namna gani Kampuni hiyo inavyothamini nguvu za vijana hasa Wanamitindo pamoja na ubunifu wa Mavazi na kwa Mara nyingine Tena wanatoa udhamini kwa Jukwaa la Mbunifu wa Mitindo Remtulah 101.

"Tunathamini na kuheshimu kazi za Sanaa hivyo kwa upande wa Sanaa hii ya ubunifu wa Mavazi tumeshiriki mara kwa mara katika kutoa udhamini ili kuhakikisha linafanyika na vijana wanaonyesha vipaji vyao kwa kubuni Mavazi yao."

Pia ametoa wito kwa vijana kuthamini na kuheshimu majukwaa mbalimbali yanayoandaliwa kama fursa kwao ili kuwapa moyo waandaji hao kuendelea kwa vizazi vijavyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...