Wa kwanza kushoto ni Dkt. Jim yonazi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya habari,technolojia na mawasiliano ,Mkuu wa Idara ya TEHAMA Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ,Raymond Machari akipokea tuzo kutoka Kwa Katibu Mkuu , Wizara ya habari,technolojia na mawasiliano Dkt. Zainab Chaula.




Na.Vero Ignatus,Arusha

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imepata tuzo ya taasisi ya afya inayoongoza kwa matumizi ya tehama kwenye utoaji wa huduma na shughuli za kila siku.

Tuzo hiyo imetolewa wakati wa mkutano wa tano wa tehama uliofanyika jijini Arusha ukiandaliea na Tume ya Tehama.

JKCI imepata tuzo hiyo baada ya Tume ya Tehama kufanya ukaguzi na kubaini kuwa asilimia 90 ya huduma za taasisi hiyo zinatolewa kwa mifumo ya tehama.

Mkuu wa Idara ya Tehama JKCI Raymond Machari amesema taasisi hiyo imejiwekeza katika kutumia tehama katika kila huduma.

“Pale JKCI kuanzia mgonjwa anapofikishwa ataandikishwa kwa mfumo wa tehama, njia hiyo hiyo itatumika anapokwenda kwa daktari hadi kufikia hatua ya kuchukua dawa.

“Ukiacha hilo pale tuna mfumo wa kufuatilia malalamiko, changamoto yani kuna namba maalum endapo mgonjwa amefika labda ameombwa rushwa au hajapatiwa huduma,” amesema Machari.

Kando na hilo taasisi hiyo pia ina mfumo unaowafuatilia na kuwakumbusha wagonjwa wake kuhudhuria kliniki.

“Kuna utafiti ulifanyika ukaonyeshwa watu wengi wanapoteza maisha kwa kutokamilisha matibabu na matumizi ya dawa.

“JKCI tukaona tuwe na mfumo ambao utatuwezesha kuwakumbusha wale wagonjwa wetu wanaokuja kliniki. Yani kama kliniki ni kesho leo mgonjwa anapata ujumbe kwenye simu yake,”. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...