Waziri wa kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akiwa ameambatana na Waziri wa Mazingira, Kilimo na Uvuvi wa Burundi Mhe. Dkt Rurema Deo-Guide wakikagua baadhi ya mazao ambayo yamefanyiwa utafiti na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Nchini Burundi ya Isabu, Tarehe 20 Octoba 2012.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Burundi
Tanzania ina uhusiano mzuri na majirani wake na katika miaka ya hivi karibuni imekuwa mshiriki kwa ukamilifu katika juhudi za kuhimiza usuluhilishi wa migogoro kwa njia ya amani.
Tanzania ni mwanachama wa vikundi vya kimataifa na kikanda pia inashiriki kwa dhati katika ushirikiano wa baina ya nchi na ushirikiano wa kimataifa.
Tanzania pia ilisaidia mazungumzo ya amani kumaliza mgogoro nchini Burundi ambapo mazungumzio hayo yalifanyika Jijini Arusha.
Serikali ya Tanzania imeendelea na juhudi zake za kuimarisha ushirikiano na nchi jirani ikiwemo Burundi ambapo pamoja na mambo mengine imekusudia kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya kilimo.
Kufuatia ushirikiano huo Waziri wa kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda amefanya ziara ya kikazi nchini Burundi ambapo aliwasili Tarehe 18 Octoba 2021 na kuanza ziara ya siku mbili tarehe 19-20 Octoba 2021.
Pamoja
na mambo mengine katika ziara hiyo Waziri Mkenda amekutana na kufanya
mazungumzo na mwenyeji wake amekutana
na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mazingira, Kilimo na Uvuvi wa Burundi Mhe.
Dkt Rurema Deo-Guide
Akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Ngozi na Kayanza alipotembelea kujionea mashamba ya Kilimo cha mahindi (Block Farming) pamoja na kutembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Nchini Burundi ya Isabu, Waziri Mkenda amesema kuwa lengo la ziara yake katika maeneo hayo ilikuwa ni kujionea hali ya ubora wa mazao ya wakulima yanayotumia mbolea ya FOMI.
“Tumekutana na wanasayansi wa hapa Burundi ili kuzungumza nao waweze kutueleza kuhusu utafiti walioufanya wa mbolea ya FOMI ili kujiridhisha kabla ya kuingia makubaliano ya kuanza matumizi ya mbolea hiyo kule nchini kwetu” Amekaririwa Waziri Mkenda
Waziri
Mkenda amemuhakikishia mwenyeji wake ambaye ni Waziri wa Mazingira, Kilimo na
Uvuvi wa Burundi Mhe. Dkt Rurema Deo-Guide
Amesema kuwa viongozi wakuu wa nchi zote mbili Tanzania na Burundi wamekuwa wakijenga uhusiano mzuri wa Kidiplomasia na kisiasa kwani wananchi wameendelea kufanya biashara za mazao bila vikwazo hususani mazao ya mahindi, mchele na Parachichi.
“Tuna kazi kubwa sisi kama serikali kuimarisha mahusiano makubwa ya kibiashara na uchumi kama ambavyo viongozi wetu wanafanya, nasi tumekubaliana kushirikiana katika sekta ya utafiti wa mazao” Amesisitiza Waziri Mkenda
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...