Na Khadija Kalili, Kibaha
Serikali Mkoa wa pwani imesaini mkataba wa kazi za ujenzi za barabara za TARURA na Kampuni 17 huku kiasi cha Bil.43.3 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi huo wa barabara ikiwa ni ongezeko la bajeti mara 4 ya bajeti ya mwaka wa fedha 20/21.
Akizungumza Wilayani Kibaha Mkoani Pwani wakati akishuhudia hafla ya utiaji saini wa mkataba huo uliyofanyika kati ya TARURA na makampuni 17 yaliyoshinda zabuni hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge ameagiza fedha hizo kusimamiwa vizuri pamoja na kuwataka wakandarasi kumaliza kazi kwa wakati uliopangwa.
Akisoma taarifa ya TARURA Meneja wa TARURA Mkoa wa Pwani Mhandisi Leopold Runji amesema mkataba huo unaenda kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii na mawasiliano na kukuza uchumi wa Mkoa wa Pwani na taifa kwa ujumla.
Naye Mhandisi Angela Shayo Akizungumza kwa niaba ya Wahandisi wengine kutoka Kampuni ya Isimila Limited alisema kuwa wao kama wakandarasi watahakikisha wanakamilisha kazi kwa wakati na kutimiza wito wa kwenda na wakati kama jinsi walivyoelekekezwa na RC Kunenge.
Hata hivyo jumla ya Bil 6.3 zimesainiwa ambapo TARURA Mkoa wa Pwani wamepokea kiasi cha shilingi Bil.2.3 kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya miundo mbinu ya barabara za Mkoa wa Pwani ambapo bajeti hiyo kwa TARURA inaenda kuongeza urefu wa barabara kutoka urefu wa KLM 57 za sasa mpaka KLM 74 sawa na ongezeko la KM 17 ambalo ni zaidi ya asilimia 29 mwaka wa fedha 21/22.
Wakati huohuo RC Kunenge amewaagiza wakandarasi hao kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa barabara hizo na kuzikamilisha kwa wakati muafaka.
"Kamilisheni barabara hizi kwa wakati mliopewa Mimi kama Kiongozi wenu katika ngazi ya Mkoa nawaheshimu kilammoja kwa fani yake hivyo nawaaahidi kuwa nitakuwa nafanya ziara za kushtukiza katika maneno yenu ya kazi ili kuona namna kazi zinavyofanyika hata kama itakua ni usiku wa manane nitapita kuwakagua " alisema RC Kunenge.
Aidha aliongeza kwa kuwaasa wakandarasi hao kuwa ni marufuku kutoa fedha kwa mtu yeyote yule hata kama atasema kuwa wametumwa na RC kumbukeni kuwa mafanikio ya kupata fedha hizi za miradi imetokana na juhudi zenu binafsi na siyo vinginevyo nasema haya na Taasisi ya Kuzuia na Kupambania na Rushwa wananisikia" alisema RC Kunenge.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...