Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Bagamoyo


KAMPUNI ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania(TGDC) ambayo ni kampuni tanzu ya shirika  la ugavi wa umeme Tanzania (TANESCO) inayoko chini ya Wizara ya Nishati imefafanua kwa kina shughuli inazofanya katika kuhakikisha inatoa mchango wake katika kuzalisha umeme unaotokana na jotoardhi nchini.

TGDC imetoa ufafanuzi wa shughuli zake kupitia mafunzo maalumu yaliyoandaliwa na Shirika la HakiMadini kwa waandishi wa habari nchini ambao wamepiga kambi wilayani Bagamoyo wakiendelea kunolewa kuhusu nishati jadidifu huku warsha ikiongozwa na mada inayosema Nishati Jadidifu kwa Maendeleo ya Uchumi na Jamii.

Akizungumza wakati akitoa mada kwa waandishi wa habari Mhandisi Cynthia Kuringe amesema TGDC ilianzishwa kwa madhumuni ya kuharakisha ya undelezaji wa rasilimali ya jotoardhi nchini.

Akieleza kwa kina kuhusu TGDC, Mhandisi Kuringe amesema kampuni hiyo inalo jukumu la kutafiti, kutathmini na kuhakiki uwepo wa rasilimali nchini, kuandaa na kutekeleza miradi ya jotoardhi ya kuzalisha umeme, kubuni na kuendeleza miradi mbalimbali itumiayo rasilimali ya jotoardhi moja kwa moja pamoja na kuishauri serikali juu ya vyanzo nafuu vya fedha za uendelezaji jotoardhi. TGDC ina mamlaka ya kutafiti ,kuchimba na kutumia rasilimali za jotoardhi nchini katika kuzalisha umeme na matumizi mengineyo. Hii itasaidia kuongeza vyanzo jadidifu nchini katika kuzalisha umeme wa uhakika vikiwemo vyanzo vingine jadidifu kama biomasi, upepo na jua.Ni nishati ya uhakika,yenye gharama nafuu na rafiki wa mazingira.

Aidha amesema kwasasa TGDC iko katika hatua ya uhakiki wa rasilimali kwa miradi ya Ngozi, Songwe, Kiejo Mbaka na Luhoi  pamoja na miradi ya matumizi mengine (direct use applications) kwa eneo la Songwe. Shabaha ni kuzalisha MW 200 za umeme kwa mwaka 2025. Jotoardhi ni rasilimali ya kimkakati na yenye kutoa fursa mpya za maendeleo ya kiuchumi na kijamii hapa nchini.


Mtalamu wa masuala ya Nishati Mhandisi Arthur Karomba akilezea mada mbalimbali kuhusu umeme jua wakati wa warsha ya kuwajengea uelewa wa sekta ya Nishati Jadidifu na Maendeleo ya Jamii waandishi wa habari iliyoandaliwa na HakiMadini kwa kushirikiana na wataalamu wa sheria kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam pamoja na Wizara ya Nishati kuhusu utafiti wa fursa na changamoto za nishati jadidifu na mchango wake katika kukuza uchumi wa nchi.

Mwandishi wa Habari na Mtangazaji kutoka TBC Zaujia Swalehe akichangia jambo kuhusu nishati jadidifu kwa maendeleo ya uchumi na jamii.

Mhandisi Cynthia Kuringe akizungumza kuhusu Kampuni yao inavyotekeleza majukumu yake katika kuhakikisha inachangia katika kuzalisha umeme unaotokana na Nishati Jotoardhi wakati wa smina iliyoandaliwa na Shirika la HakiMadini kwa ajili ya waandishi wa habari kujengewa uelewa kuhusu masuala yanayohusu nishati jadidifu.
Mwandishi kutoka gazeti la Mwananchi Halili Letea,akifafanua jambo wakati wa semina iliyoandaliwa na Shirika la HakiMadini inayoendelea wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Mwandishi kutoka Gazeti la Nipashe Salome Kitomari akizungumza mbele ya washiriki wa semina hiyo.

Mwandishi wa habari kutoka gazeti la Jamvi la Habari Hafidhi Kido akichangia hoja wakati wa semina ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na Shirika la HakiMadini.

Mjiolojia John Bosco (kulia) akijadiliana jambo na Mratibu wa Mradi kutoka Shirika la HakiMadini wakati wa semina kwa waandishi wa habari.Semina hiyo imejikita kujadili Nishati Jadidifu kwa Maendeleo ya Uchumi a Jamii.

Mkurugenzi Mkuu wa Rift Valley Energy Deo Massawe akifuatilia mjadala wakati wa semina iliyoandaliwa na Shirika la HakiMadini kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini.

Profesa Majombo kutoka Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM)akifafanua jambo wakati wa semina hiyo.

Mkufunzi kutoka HakiMadini akitoa mada wakati wa semina hiyo iliyohusu Nishati Jadidifu na Maendeleo ya Jamii.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...