Na Sixmund J. Begashe

Wataalam wa Makumbusho ya Taifa kutoka Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Idara ya Program wakiongozwa na Mkuu wa Idara hiyo Bw Chance Ezekiel, wamekutana na kufanya mazungumzo na Mwambata wa Utamaduni wa Ubalozi wa India nchini Mhe Santhosh G.   Raja  kwenye kituo cha Utamaduni cha Ubalozi huo Dar es Salaam

Akizungumzia kikao hicho Bw Ezikiel amesema kimelenga kuboresha onesho la Mwezi huu la Museum Art Explosion kwa kuwa litashirikisha kikundi cha Sanaa cha Baba Gorenath Gptipua kutoka nchini India pamoja na wa hapa nchini.

"India na Tanzania zinatimiza miaka 60 ya mashirikiano, hivyo kupitia program yetu ya kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi tumeona ni vyema tushirikishe wasanii kutoka India kama sehemu ya kuonesha uimara wa udugu wetu kupitia sanaa na Utamaduni." Bw Ezekiel

Bw. Ezekiel aliongeza kuwa Maonesho ya mwezi huu yanayo tarajiwa kufanyika tarehe 29/10/2021 siku ya Ijumaa yatakuwa ya kipekee sana maana watoto wa kitanzania na jamii ya Wahindi waishio nchini wataonesha umahiri wao katika kazi za sanaa za ufundi na wasanii wa "Jambo na Vijambo" wa hapa nchini na kikundi cha Baba Gorenath Gptipua kutoka India wataonesha umahiri wao jukwaani.

Akielezea maandalizi ya kikundi cha sanaa kutoka nchini India Mhe. Raja  amesema watanzania wawe tayari kupata burudani nzuri kwani wasanii wapo tayari na wanauzoefu mkubwa wakufanya maonesho kimataifa. 

"Wasanii wamejiandaa vizuri sana, sisi kama Ubalozi tumesha waandalia mapokezi mazuri, na niipongeze Makumbusho ya Taifa kwa kuanzisha program hii ambayo inatoa nafasi kwa watanzania kupata ladha tofauti ya kazi za sanaa." Aliongeza Mhe Santhosh.

Program ya Museum Art Explosion inayofanyika kila Ijumaa ya mwisho wa Mwezi, kwa mwezi huu imetoa nafasi kwa wasanii chipukizi kuonesha kazi za sanaa za ufundi na wasanii wa Jambo na Vijambo pamoja na kutoka India kuonesha sanaa za jukwaani kama Maigizo, Ngoma, muziki, sarakasi, vichekesho nk.

Katika ni Mwambata wa Utamaduni wa Ubalozi wa India nchini Mhe Santhosh G. Raja akiendesha kikao kati kituo cha Utamadini cha nchi hiyo na wajumbe wa kamati ya Museum Art Explosion, Dar es Salaam
Katika ni Mwambata wa Utamaduni wa Ubalozi wa India nchini Mhe Santhosh G. Raja akiwaonesha wajumbe wa kamati ya MAE eneo la maonesho ya jukwaani ya kituo hicho.
Mkuu wa Idara ya Program Bw Chance Ezekiel akifafanua jambo kwa Mwambata wa Utamaduni wa Ubalozi wa India nchini Mhe Santhosh G. Raja

 Kushoto ni Mwambata wa Utamaduni wa Ubalozi wa India nchini Mhe Santhosh G. Raja akielezea kwa wajumbe wa kamati ya Museum Art Explosion (MAE) vifaa vya muziki wa asali, katikani ni Mkuu wa Idara ya Program Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Bw Chance Ezekiel na kulia ni Mjumbe wa MAE Bw Anastasius Liwewa


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...