kutoka kulia ni Sajenti Juma Mabeyo ,Mkaguzi wa magari na msaili wa madereva kutoka mkoa wa Manyara akionyesha baadhi ya vifaa wanavyotumia kwenye zoezi la ukguzi wa magari  (aliyeshika kioanzasauti)Sajenti Paschal Kimario  ,Mkaguzi wa magari na msaili wa madereva kutoka mkoa wa Arusha akitoa ufafanuzi kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa John Mongela
wa kwanza kushoto ni Mkaguzi wa magari sanjenti Paschal Kimaro akitoa maelezo juu ya vifaa vya kukaguliwa magari kwa mgeni rasmi  ambaye ni mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela,kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo
kutoka kulia ni Sajenti Juma Mabeyo ,Mkaguzi wa magari na msaili wa madereva kutoka mkoa wa Manyara (aliyeshika kioanzasauti)Sajenti Paschal Kimario  ,Mkaguzi wa magari na msaili wa madereva kutoka mkoa wa Arusha akitoa ufafanuzi kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa John Mongela
Mkuu wa mkoa John Mongela akiangalia z basi la Abiria ambalo limefanyiwa ukaguzi katika uzinduzi wa zoezi la ukaguzi wa vyombo vya Moto  katika viwanja vya soweto  Jijini Arusha 

Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela akizungumza na wadau wa  usafirishaji katika uzinduzi wa ukaguzi wa vyombo vya Moto uliofanyika katika viwanja vya soweto Jijini Arusha 
Mkuu wa Usalama barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu wa polisi Solomon Mwangamilo,akizungumza katika uzinduzi wa ukaguzi wa vyombo vya Moto katika viwanja vya soweto Jijini Arusha,kulia kwake ni mwenyekiti wa Kamati ya Usalama barabarani Gelace Rutachubirwa 

UZINDUZI WA ZOEZI LA UKAGUZI WA VYOMBO VYA MOTO WAFANYIKA ARUSHA

 Na Vero Ignatus,Arusha

Uzinduzi wa ukaguzi wa vyombo vya Moto imefanyika rasmi Jijini Arusha,ukiwa na lengo la kutoa Elimu kwa Jamii kuelekea maadhimisho ya wiki ya nenda  kwa usalama barabarani ambayo Kitaifa yatafanyika mkoani Arusha kuanzia tarehe 15.11.2021 hadi tarehe 20.11.2021.

 Mkuu wa Usalama barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi Solomon Mwangamilo ,akitoa taarifa fupi kuhusiana na maadhimisho hayo alisema lengo ni kutoa nafasi kwa Baraza la Usalama barabarani ,kufanya tathmini ya jumla kwa mwaka mzima ,kuhusiana na usalama wa watumiaji wa vyombo vya moto, kuangalia maeneo ambayo yanapelekea ajali nyingi za barabarani na kuja na mikakati ya kupunguza ajali hizo.

Mwangamilo alisema wataendelea  watatoa elimu ikiwa ni pamoja na kukagua vyombo vyote vya moto vilivyopo mkoani Arusha, ambapo wametenga maeneo tofauti kwa ajili ya zoezi hilo kwa kuzingatia ukubwa wa Jiji, zoezi litafanyika katika vituo vya Polisi, viwanja vya Soweto na kwa upande wa wanaomiliki idadi kubwa ya vyombo vya moto watapeleka Wakaguzi wa magari kwenda kufanya ukaguzi katika maeneo yao, baada ya kupokea maombi lengo likiwa ni kupunguza ucheleweshwaji wa utoaji huduma.

Kwa upande wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo ,wakati akimkaribisha Mkuu wa Mkoa alisema kama Watumiaji wa vyombo vya moto watafuata kauli mbiu ya utii wa Sheria bila shuruti watapunguza ajali nyingi za barabarani ambazo zimepelekea watu wengi kupoteza maisha, ulemavu pamoja na uharibu wa vyombo vya moto.

 Akizungumza mgeni rasmi katika uzinduzi wa zoezi hilo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela, ameanza kwa  kulipongeza Jeshi la polisi kupunguza matukio ya ajali za barabarani,pamoja  na ubunifu wa kwenda katika maeneo ya wanaomiliki idadi kubwa ya vyombo vya moto ,kwa ajili ya kukagua vyombo vyao.

Mongela alisema ni muhimu Wananchi waendelee kuelimishwa, kuhusiana na sheria za usalama barabarani,na kukemea vitendo vya rushwa kwa Askari wachache ambao wanachafua taswira ya Jeshi la Polisi.

Niwapongeze wadau wa usalama barabarani,  hususani madereva kwa kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya ukaguzi wa vyombo vyao,niliombe Jeshi la polisi kupitia Kitengo Cha Usalama barabarani zoezi hili liwe na ufanisi lisigeuke kuwa kero,na kuzalisha malalamiko.alisema

Jeshi la polisi ndio msingi wa Dola na mmepewa jukumu la moja kwa moja kukutana na changamoto za  wananchi pamoja na malalamiko yao,hatuhalalishi kero Ila nasema wakati mwingine,ukindoa  wale wachache ,ambao wanaosababisha kero zisizo za msingi ya kutokua na uadilifu 

Mongela alisisitiza kuwa kutoa Elimu isiwe kwa wananchi na wadau wa nje pekee, bali hata  ndani ya Jeshi la Polisi lenyewe,ili kukumbushana  wajibu na viapo vyao,ili kuweza kuwa wasafi zaidi na kuepukana malalamiko na  lawama zipungue.

"Wakati inapobidi tuchukue hatua maana unajua Kuna mtu kazaliwa mtukutu na kadhapenya Sasa na kila unavyofanya wewe unakuwa Kama unsmchochea, anafanya zaidi,Sasa hatua zichukuliwe kwasababu mwisho wa siku Jeshi zima linaonekana Kama linatatizo kumbe ni watu wachache tu"Alisema Mongela

Alimaliza kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuelekeza maadhimisho hayo kitaifa yafanyike Mkoa wa Arusha, hivyo akatoa wito kwa wadau wa usalama barabarani kushikama na kujitoa kwa pamoja  ili kuhakikisha maadhimisho hayo yanafanyika kwa hali ya amani na utulivu


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...