NA FARIDA SAIDY,KILOMBERO.
Viongozi wa madhehebu ya dini Mkoani Morogoro
wamewataka waumini wa madhehebu yao na watanzania kwa ujumla kuacha tabia ya
kulalamikia viongozi wa Serikali badala yake wawape muda wa kutekeleza majukumu
yao huku wakiwaunga mkono kwa kufanya kazi za kujiingizia kipato sambamba na
ulipaji kodi bila shuruti.
Wito huo umetolewa wilayani Kilombero na Askofu Mkuu
wa makanisa ya free pentekoste Tanzania
FPCT Askofu Stivine Mulenga,wakati wa hafla ya kumsimika askofu mpya wa jimbo
la kilombero.
Askofu Mulenga amesema kuwa ni muda sasa wakuacha
kuitupia Serikali lawama badala yake kufanya kazi kwa bidii na kushrikiana na
Serikali ili kukuza uchumi wa nchi hali itakayosaidia kubadilisha maisha ya
kila moja hapa nchini.
“Ni lazima tuwape muda viongozi wetu,hata
ukimuchagua wa chama kingine hawezi kufanya kazi unavyotaka wewe lazima achague
upande sahihi”.Alisema askofu Mwanga.
Aidha amewataka waumini kuwaheshimu viongozi wao
pamoja na kuwaombea viongozi “kwani neno la mungu linasema lazima tuiombee
serikali na viongozi wake” .Alisema Mwanga.
Kwa upande wake Askofu Mstaafu wa Kanisa la
Kipentekoste Jimbo la Kilombero Askofu Lameck Bwango naye alikuwa na haya ya
kusema
Nao wamumini na wa kanisa hilo akiwemo Barnabas Bwango na Esther Mkwazu wamewataka vijana kufanya kazi kwa nguvu zao zote ili kuondoa malalamiko ya ugumu wa maisha na ukosefu wa ajira
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...