Na. John Mapepele

Mabingwa watetezi wa Mashindano ya Afrika kwa mchezo wa Mpira wa Miguu kwa wenye Ulemavu CANAF 2021 timu ya Angola leo, Novemba 28, 2021 wameonyesha kwamba wao ni mabingwa wa dunia katika mchezo huu baada ya kuichabanga Zanzibar dazani moja kwa nunge kwenye Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.

Katika kipindi chote Angola waliutawala mchezo huo kutokana na uzoefu mkubwa wa wachezaji wao wanaocheza katika mashindano ya kimataifa.

Kipindi cha kwanza tayali Angola ilikuwa inaongoza kwa magoli sita kwa nunge na katika kipindi cha pili wakaongeza magoli mengine sita na kufanikiwa kupata ushindi wa dazani moja kwa sifuri dhidi ya timu ya Zanzibar.

Magoli ya Angola yamefungwa na Kufula Hilario, Aharo Francisco, Joachim Sabino, Chiarere Jord na Pacincia Fblio.

Wakati huo huo katika mchezo mwingine, Timu ya Siera Leon imeibamiza mabao 3- 0 ambapo bao la kwanza limefungwa katika dakika ya 15 na mshambuliaji Kuroma Ctbassy na goli la pili limefungwa dakika ya 18 ya kipindi cha kwanza na goli la tatu dakika ya 43 kipindi cha pili na Lumeh Foday.

Mchezo huo ulitawaliwa na mvua kubwa hali iliyosababisha kushindwa kuendelea na kwa muda baada ya kipindi cha kwanza cha mchezo kumalizika kutokana na maji kujaa katika uwanja.

Mashindano haya yamezinduliwa rasmi jana Novemba 27 na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa na yatakamilika Disemba 4, 2021.

A.  Wachezaji wa Angola (jezi nyekundu) wakikabiliana na wachezaji wa Zanzibar (jezi ya kijani mpauko) kwenye mchezo wa CANAF 2021 uliochezwa leo, Novemba 28,2021 jijini Dar es Salaam ambapo Angola imeshinda 12-0.

Timu za Uganda (jezi nyekundu) na Timu ya Siera Leon (jezi nyeupe) wakiimba nyimbo zao za Taifa wakati wa mechi ya mashindano ya CANAF 2021 leo Novemba 28, 2021

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...