Mkurugenzi Mkuu wa
Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mhandisi Dkt.
Samuel Gwamaka afanya ziara katika safu
ya milima ya livingstone Wilaya ya Kyela
Kata ya Matema Mkoani Mbeya na kubaini
Kuna uchomaji moto katika milima hiyo na
kusababisha uchafuzi mkubwa wa Mazingira na uoto wa asili kupotea.
Dkt. Gwamaka akiwa
katika Kijiji cha Ikombe eneo la lyulilo amezungumza na wananchi wa Kijiji hiko
na kuwaeleza kuwa shughuli za uchomaji moto katika milima hiyo ni uharibifu wa
Mazingira na unaathari kubwa kwa viumbe hai wanaoishi katika Hifadhi ya milima
hiyo.
Aidha ameendelea kusema
kuwa Milima ya Livingstone inagusa Mikoa mitatu ikiwemo Njombe ,Iringa na Mkoa
wa Mbeya hivyo inapaswa kuwa na ushirikiano kati ya Mikoa hiyo ili kuweza
kupambana na uharibifu wa Mazingira katika milima hiyo. Amesema kuwa Baraza
linaendelea kutoa elimu kwa jamii ili
wafahamu kuwa madhara ya uchomaji moto
katika milima hiyo ni makubwa kwani itaathiri kizazi kilichopo na kijacho, kama
tunavyoona hali iliopo sasa joto limeongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na
ukataji miti hovyo. Pia itambulike kuwa milima hiyo ndio kichocheo kikubwa cha
upatikanaji wa maji katika mito yetu hivyo kunahaja ya kutunza na kuilinda
"Niwaombe wananchi
wa Kijiji hiki na vingine kuhakikisha wanashirikiana na Serikali katika kusimamia hifadhi ya
milima ya Livingstone ili kukilinda kizazi chetu na Taifa letu kwa ujumla. Kama
tulivyo msikia Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan
Suluhu akisisitiza Kila Halmashauri kupanda miti million 1.5 na sio kupanda tu
bali ni lazima miti hiyo itunze ili kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Hivyo mazingira ni yetu sote tuhakikishe tunashirikiana na mamlaka husika kama
Wakala wa Misitu na Mamlaka ya Hifadhi ya wanyama pori ili kuendelea
kuhakikisha maeneo ya Misitu na Hifadhi tunaendelea kulinda kwa Mustakabali wa
Nchi yetu pamoja na vizazi vinavyokuja" Amesema Dkt. Gwamaka
Kwa upande wake
Mtendaji wa Kata ya Matema Bw. Charles Mwamamba amemshukuru Dkt. Gwaka kwa ujio
wake kwani imeongeza nguvu kwa jamii na wananchi wa kijiji cha Ikombe na
amesema kuwa matumaini yake elimu aliyotoa kwa wana kijiji hao itasaidia
kuelewa kuwa wanapochoma moto wanasababisha madhara makubwa sana katika
Mazingira. Ameendelea kusema kuwa historia ya Milima ya Livingstone ilikuwa na
uoto wa kutosha lakini shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo, ukataji miti kwa
ajili ya mkaa pamoja na uwindaji ndio zilizopelekea uharibifu huo kutokea.
Naye Meneja wa Kanda
Nyanda za Juu Kusini NEMC Bi.Glory Kombe amesema kuwa milima ya Livingstone ni
maeneo muhimu sana ambayo yanahitaji kuhifadhiwa hivyo sisi kama NEMC
tutashirikiana na Halmashauri ya Njombe, Rudewa, Makete Rungwe na Kyela
kuhakikisha tatizo hili la moto kutotokea tena kwa miaka ijayo na tutahakikisha
milima hii inaifadhiwa ipasavyo. Pia tutahakikisha Sheria ya Mazingira
inatekelezwa na kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika wanafanya uharibifu
wa Mlima huu.
1.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mhandisi Dkt. Samuel Gwamaka pamoja na
watumishi wa NEMC Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wakiwa katika picha ya Pamoja
na Prof. Mark Mwandosya walipofanya ziara Wilaya ya Kyela katika Safu ya Milima
ya Livingstone.
1. Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mhandisi Dkt. Samuel Gwamaka akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ikombe Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya kuhusu uchomaji moto katika Milima ya Livingston.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...